Baadhi ya maafisa waandamizi/ makatibu wakuu wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo
Jijini Dar es Salaam
Washiriki wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam wakifuatilia mkutano huo
Baadhi ya mawaziri wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof Palamagamba kabudi (Mb) (wa kwanza kushoto) akiongea na wajumbe wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam
Baadhi ya mawaziri pamoja na maafisa waandamizi/ makatibu wakuu wakifuatilia mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika kwa njia ya (Video Conference) leo Jijini Dar es Salaam.
*************************************
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini
mwa Afrika (SADC) wamakaa kikao kwa njia ya mtandao na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo hatua ambazo wamezichukua kutekeleza miongozo na maamuzi ambayo waliyafanya kuhusu kupambana na maradhi ya Covid-19 ambapo walikubaliana kuendelea kuruhusu usafirishaji wa bidhaa muhimu na huduma katika Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC.
Akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC kwa njia ya Video katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof Palamagamba kabudi amesema kuwa wote kwa pamoja wamkubaliana kuwapongeza na kuwashukuru madereva wa maroli yanayopeleka bidhaa katika nchi mbalimbali kwa kazi nzuri wanayoifanya.
“Sisi tumeanza kwanza kuwa na miongozo kumekuwa na changamoto za hapa na pale ambazo sasa tumekubaliana kwa pamoja na changamoto hizo katika utekelezaji wa kanuni hizo na miongozo hiyo sasa uende kwenye kamati ya pamoja ya wataalamu itakayoongeza wajumbe ile ya afya ili kupitia changamoto mbalimbali ambazo zimejitokeza wakati wa utekelezaji huo ili kuhakikisha kwamba sasa changamoto hizo tunazitatua ili kuhakikisha kwamba tunakuwa na mtiririko wa bidhaa na huduma muhimu kwa haraka iwezekanavyo wakati wa utekelezaji”. Amesema Prof.Kabudi.
Aidha Prof.Kabudi amesema kuwa wakati hatua za kukabiliana na janga la Corona zikiendelea kuchukuliwa
nchi za SADC lazima zikumbuke dhumuni la utangamano miongoni mwa nchi wanachama ambalo ni kuboresha ufanyaji biashara baina ya nchi na nchi na hivyo kutowaangusha waanzilishi wa Jumuiya ya SADC.
“Madereva wetu wamevunjika moyo kwa sababu wanaonekana kama wao ndio wanaosambaza virusi vya Corona na sio askari wazuri ambao wanatoa huduma ya
kusafirisha huduma na biidhaa muhimu wakati huu wa mlipuko, katika nchi za jumuiya,”. Amesema Prof.Kabudi.
Pamoja na hayo Prof.Kabudi amesema ufanyikaji wa biashara baina ya nchi na nchi ndani ya SADC uko chini ya
asilimia 20 hali ambayo inazuia nchi wanachama kuona ukuaji wa uchumi wake na kuongeza kuwa janga la corona lichukuliwe kama kichocheo cha kuongeza juhudi za kuinua kaiwangi cha ufanyaji wa biashara baina ya nchi na nchi kupitia utekelezajia wa Protokali ya SADC katika biashara ya 2005 na uanzishwaji w eneo huru la biashara la SADC.
Ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Isack Kamwele, Waziri wa Maliasilia na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala na Waziri wa
viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa.
Nchi zinazoshiriki Mkutano huo ni Angola, Afrika Kusini, Botswana, Malawi, Lesotho Comoro, Eswatini, Mauritius, Msumbiji, Madagascar, Namibia, Visiwa vya Shelisheli, Zambia, Zimbabwe na Mwenyekiti Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.