Home Mchanganyiko RC MAHENGE AWATAKA TEMESA KUTATUA CHANGAMOTO YA MFUMO WA UMEME KATIKA HOSPITALI...

RC MAHENGE AWATAKA TEMESA KUTATUA CHANGAMOTO YA MFUMO WA UMEME KATIKA HOSPITALI YA RUFAA DODOM

0

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge akizungumza na watumishi mara baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Best Magoma akitoa maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge (hayupo pichani) ambaye alifanya  ziara ya kikazi ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali Ya Mkoa wa Dodoma,Dkt. Ernest Ibenzi,akizungumza kwenye ziara ya  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge (hayupo pichani) ambaye alifanya  ziara  katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Idara ya Meno Hospitali ya Dodoma Atanas Masele,akielezea changamoto zinazopatikana katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Muonekano wa mashine ya mionzi (X-Ray) iliyopo katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge akikagua mashine baada ya kufanya ziara ya kikazi ya kushtukiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

………………………………………………………………………………….
Na. Alex Sonna, Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge amemta Katibu Tawala wa Mkoa huo kuwaita wataalamu wa TEMESA kufanya uchunguzi na tathimini juu ya kutatua changamoto ya umeme katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Agizo hilo amelitoa wakati wa ziara yake ya kikazi katika hospitali hiyo baada ya kuhoji na kukuta kuna baadhi ya vifaa havitumiki kutokana na changamoto ya mfumo wa umeme kuwa mdogo.
Wataalamu hao wa TEMESA wanatakiwa kufika hapo na kufanya uchunguzi kisha kuandika taarifa ya kilichopatikana katika uchunguzi huo na kueleza mpango mkakati juu ya kutatua changamoto hiyo kwani watanzania wanahitaji huduma kutoka katika hospitali zilizojengwa kwa kodi zao.
“ Hatuwezi kuwa na wataalamu TEMESA harafu tukashindwa kurekebisha miundombinu ya mfumo wa umeme ili watanzania kupata huduma bora wanayotegemea kupata kutoka katika serikali yao”, ameeleza Dkt. Mahenge.
 Dkt. Mahenge ametoa wito kwa wahudumu wa afya kutoa taarifa pale wanapokutana na changamoto katika utendaji wao ili kutatuliwa kwa haraka na kuendelea kuhudumia wanachi kwa wakati.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali Ya Mkoa wa Dodoma,Dkt. Ernest Ibenzi ameeleza namna wanavyofanya kazi japo mashine ya mionzi (X-Ray)imeharibika japo amesema kuja kufikia jumatatu itakuwa imetengenezwa ili wananchi waendelee kupata huduma hiyo katika hospitali hiyo.
Naye Mkuu wa idara ya meno hospitali ya Dodoma Atanas Masele, amesema kuwa kutokana na kuwa na vifaa vipya vya kisasa kumekuwa na changamoto ya umeme kuwa mdogo hivyo walishauriwa kufanya maboresho katika mfumo wa umeme ilikuweza kurejesha huduma kwa wanachi.
“Hata hivyo tunampango wa kufanya maboresho katika miundombinu ya hospitali nzima ili kuweza kukidhi mahitaji ya watanzania kama inavyotakiwa”, amesema Masele.