Kampuni ya bia Tanzania ya Tanzania Breweries Public Limited Company kwa kushirikiana na taasisi ya Tanzania Agricultural Research Institute (TARI) zimefanya utafiti na kuibuka na mbegu bora za mtama kwa ajili ya matumizi ya uzalishaji wa bia kupitia mradi shirikishi wa kuwawezesha wakulima wa zao la mtama nchini.
Mradi huo umelenga kuongeza uzalishaji wa zao la mtama nchini
Kupitia mradi huo mbegu zinazalishwa kwa kutumia utaalamu wa kisasa ambao unawezesha kuongeza mavuno kwa asilimia 43% tofauti na uzalishaji unaotumika kwa kutumia njia nyinginezo.
Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Philip Redman amesema amesema kuwa anaamini utafiti utafiti za uzalishaji mbegu bora ulionza kufanyika mwezi Desemba mwaka jana katika maeneo ya Hombolo, Kibaigwa na Kongwa mkoani Dodoma na utafanikisha kupata mbegu bora za mtama kwa ajili ya kusambaza maeneo mengineyo nchini.
“Kupitia mradi huu,wakulima wa mtama wataweza kupatiwa ushauri wa kilimo bora kutoka kwa wataalamu wetu na lengo letu kubwa ni kuwawezesha wakulima wa mtama kupata mavuno mengi zaidi,kutumia maji kidogo na kuwawezesha kuwa na bima ya kuwakinga na changamoto za kilimo”alisema.
Redman alisema mbali na kulenga kuinua maisha ya wakulima kampuni pia inategemea kupata malighafi ya uzalishaji wa bia zake za gharama nafuu za Eagle Lager na Bingwa.Kampuni tayar imejipanga kununua asilimia 74% ya malighafi nchini na itaendelea kununua malighafi zake zote kutoka hapa nchini katika kipindi cha miaka ijayo.
Kwa upande wake,Meneja wa mradi wa TARI wa Hombolo, Dk. Lameck Makoye, alisema kuwa kuwa mradi huu utawezesha wakulima kupata mbegu bora za mazao ambazo zinawawezesha kupata mavuno zaidi ya mtama na kuboresha maisha yao.