Home Mchanganyiko VODACOM YAENDELEA KUWEZESHA WATEJA WAKE KWA KUTUSUA MAPENE

VODACOM YAENDELEA KUWEZESHA WATEJA WAKE KWA KUTUSUA MAPENE

0
Mshindi wa wiki wa shindano la TUSUA MAPENE NA VODACOM, Neema Laiser ( katikati) mfanyabiashara, mkazi wa mtaa wa Uswahilini Jijini Arusha,  akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 toka kwa  Meneja mkakati wa Masoko Vodacom kanda ya Kaskazini, Abednego Mhagama (kulia) na Meneja Mauzo mwandamizi wa Vodacom kanda hiyo, Nathanael Pedigando
………………………………………………………………………………
Shindano la Tusua mapene na Vodacom  linaloendelea kote nchini, linawawezesha watumiaji wa mtandao wa Vodacom kuweza kujishindia kitita cha milioni 10 kila wiki na wengine waliobaki watajishindia zawadi ndogo ndogo. Hili ni shindano lilioanza mwaka 2017, na kuendelea kuwanufaisha wateja wa Vodacom nchini. 
Ili kushiriki kwenye promosheni hii, mteja anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
Unaponunua tiketi, moja kwa moja unaingia kwenye droo, washindi wa droo wanaingia kwenye Mpambano ambapo  wanatumiwa neno maalum ” keyword ” watakayoituma kwenda 15544 ili kuweza kukomboa zawadi. Wa kwanza kutuma neno hilo ataibuka na kitita cha shilingi milioni 10, na wengine wanajipatia zawadi ndogo ndogo.
Akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 za kitanzania, Meneja Mauzo mwandamizi wa Vodacom kanda ya Kaskazini, Abednego Mhagama alimpongeza mshindi na kuhamasisha wateja kushiriki Zaidi ili kuweza kujishindia zawadi kemkem.
Nae mshindi wa zawadi ya Tusua mapene kutoka Arusha mjini, Mfanyabiashara Neema Laiser aliwashukuru Vodacom kwa kuanzisha shindano hili ambalo limemuwezesha kujishindia pesa itakayomuwezesha kuongeza mtaji na hivyo kuimarisha biashara yake.
“Kwa kweli sikuamini nilipopigiwa simu nikajua mambo ya uwongo, lakini kumbe ni kweli na nawashauri watu wasiache kutumia mtandao wa Vodacom maana ushindi kama huu unaweza kukukwamua kiuchumi” alisema Laiser.