Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu
Semistocles Kaijage, akizungumza katika Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa
kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na
Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika loe 27, Mei 2020, JNICC Jijini
Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, akifafanua hoja zilizotolewa na Washiriki wa Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika leo 27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage, akiendesha Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika leo 27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Dkt. Wilson Mahera, akizungumza katika Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika leo 27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu. Humphrey Polepole akichangia hoja katika Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika leo 27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mstaafu.Francis Mutungi akifuatilia Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika leo 27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika akichangia hoja katika Mkutano wa NEC na Vyama vya Siasa kujadili na kupitisha Kanuni na Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwaka 2020, Mkutano ambao umefanyika loe 27, Mei 2020, JNICC Jijini Dar es Salaam.
Picha na Idara ya Habari-MAELEZO.
*******************************
NA EMMANUEL MBATILO
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imejizatiti na imejipanga kuhakikisha kuwa inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni pamoja na kuzingatia masharti ya Kanuni za Maadili ya Uchaguzi.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Mhe.Jaji Semistocles Kaijage katika kikao na vyama vua Siasa na Wadau wengine wa Uchaguzi kujadili na kupitisha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2020.
Akizungumza katika kikao hicho Jaji Kaijage amesema kuwa NEC kwa kushirikiana na vyama vya Siasa na Serikali huandaa Maadili ya Uchaguzi kwa shabaha ya kuwa Uchaguzi ulio huru, wa haki, wa wazi na wa kuaminika.
“Maadili yatasaidia kuwa na uwanja sawa wa ushindani katika Uchaguzi.Maadili hayo huandaliwa kwa mujibu wa kifungu Cha 124A Cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ya sheria za Tanzania kwa kuzingatia mahitaji yaliyopo”. Amesema Jaji Kaijage.
Jaji amesema kuwa ni muda mwafaka tena kwa vyama vya siasa, Tume na Serikali kama wadau wa Uchaguzi kuandaa Maadili hayo kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
“Natambua kuwa vyama na Serikali mlipewa Rasimu ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020 ambapo mlipata fursa ya kupitia na kutoa maoni na mapendekezo yenu ambayo yamezingatiwa katika Rasimu hii ya Maadili”. Amesema Jaji Kaijage.
Pamoja na hayo Mhe.Kaijage aliwaaomba Wadau mbalimbali wa Uchaguzi baada ya majadiliano hayo na kuridhiwa kwa Maadili,wahusika wataweka saini ya kuyakubali, kuyaheshimu na kuyatekeleza kuanzia wakati was kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu na chaguzi ndogo zitakazofuata.