******************************
Na Magreth Mbinga
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka wananchi wa Mkoa huo kufanya kazi ili kufidia siku ambazo wamekaa ndani.
Amezungumza hayo leo wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa standi mpya ya mabasi yaendayo mikoani na nje ya nchi pamoja na ofisi ya Wilaya ya Ubungo.
RC Makonda amesema standi hiyo itakuwa ya mfano kwa Afrika na watu wengi watakuja kwaajili ya kujionea ilivyokuwa ya aina yake.
Vilevile RC Makonda amemtaka Mkuu wa Wilaya hiyo kusimamia miradi apambane kuhakikisha inatekelezeka kabla ya June 31 ili kutekeleza ahadi ambazo zilitolewa na Mh Rais.
Sanjari na hayo Rc Makonda amesema mradi huo unaendelea vizuri japo Kuna changamoto za mvua na hadi sasa ujenzi umefikia 70% ya ujenzi ambao utaghalimu Bilioni 50.9.
Hatahivyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Bi.Beatrice Dominic amesema mpaka Sasa mradi wa jengo la ofisi ya mkuu wa Wilaya limegharimu Bilioni3 na hakuna madai ambayo yamefika mezani kwake pia mkandarasi walimuongezea muda wa miezi sita kwaajili ya kumaliza ujenzi huo.