**********************************
Na Magreth Mbinga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Paul Makonda ametembelea ujenzi unaendelea wa barabara inayoanzia Bamaga na kuishia Shekilango.
Akizungumza katika ukaguzi wa barabara hiyo RC.Makonda amesema kuwa bado anaendelea kufatilia ahadi za Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania aliahidi kuijenga ili kuona juhudi zinazoendelea kufanywa na waliokabidhiwa kukamilisha ujenzi huo.
RC Makonda amesema barabara hiyo ina urefu wa Km3.7 ambayo itakuwa na njia nne mbili kutoka Shekilango kwenda Bamaga na mbili zingine kutoka Bamaga kwenda Shekilango.
Aidha,RC Makonda amesema barabara ifungwe taa pia watengeneze njia ya watembea kwa miguu na m4 itengenezwe kama sehemu ya kivutio kwa wote watakao tumia barabara hiyo.
Sanjari na hayo RC Makonda amewataka wananchi waendelee na maombi ya shukrani ambayo yalitangazwa na Mh Rais ambayo yameanza jana ijumaa na kumalizika kesho siku ya jumapili.
“Naomba nitoe ratiba ya kesho kila mmoja afanye maombi ya shukrani kumshukuru Mungu ametusaidia tunaendelea vizuri na mapambanao ya ugonjwa huu wa Corona”amesema RC Makonda.
Hata hivyo amemalizia kwa kuwataka Wananchi wote siku ya kesho kufanya maombi ya kuwaombea marehemu wote baada ya maombi hayo washeherekee kwa shangwe kubwa.
“Kama unaweza kuchoma mbuzi choma sherehekea ,piga mziki cheza ,kwa wanaoweza kuogelea oga ,toka na familia yako mukapate chakula cha jioni kwa pamoja na DJ piga mziki mzuri ili watu wafurahi hiyo yote ni katika kusheherekea na ulinzi utakuwepo wa kutosha”amesema RC Makonda.