Home Uncategorized NIMEOMBA KUJIUNGA NA CCM, LAKINI HATA KAMA WATANIKATAA SIRUDI CHADEMA NG’OOO

NIMEOMBA KUJIUNGA NA CCM, LAKINI HATA KAMA WATANIKATAA SIRUDI CHADEMA NG’OOO

0

Aliekuwa Mbunge wa Chadema Peter Lijualikali akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo wakati akitangaza rasmi kukihama chama hicho kwa madai ya kutofurahishwa na mwenendo wake na kuomba lidhaa ya kuhamia CCM.

Aliekuwa Mbunge WA Chadema Peter Lijualikali akionesha nyaraka mbalimbali wakati akitangaza  kukihama chama hicho kwa madai ya kutofurahishwa na mwenendo wake na kuomba lidhaa ya kuhamia CCM

Baadhi ya wanahabari wakimsikiliza aliyekuwa mbunge wa Chadema Peter Lijualikali wakati akizungumza leo.

…………………………………………..

Aliekuwa Mbunge WA Chadema Peter Lijualikali ametangaza rasmi kukihama chama hicho kwa madai ya kutofurahishwa na mwenendo wake na kuomba lidhaa ya kuhamia CCM

Lijualikali amesema kwamba anaomba ridhaa ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM kama watampokea na kumpa nafasi ya kuwatumikia watanzania shughuli yoyote, lakini pia CCM wakinikataa sirudi Chadema Ng’oo.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo Mbunge wa Kirombelo Peter Lijualikalu amesema kuwa haridhishwi na mwenendo wa chama cha Chadema hali iliyosababisha kukihama   chama hicho.

Lijualikali amempongeza Raia Magufuli kwa kutotangaza hatua ya kutotangaza hatua ya Lockdown  kwakuwa ingesababisha madhara makubwa kwa taifa kwa sababu watanzania waliowengi wanategemea kipato na shughuli za kila siku,

Katika hatua nyingine Lijualikali amewasihi watanzania kutowaamini wanasiasa walaghali kwakuwa hawana nia ya dhati ya kuleta maendeleo ya nchini