*******************************
Wizara ya Kilimo imejipanga kuhakikisha mikoa mingi kujitosheleza kwa mafuta ya kula.
Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa mjini Kigoma na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Kusaya alipoongea na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Waziri Mkuu .
” Jitihada za Wizara hadi sasa tumeweza kuzalisha mbegu bora za michikichi 1,556,111 ambapo miche 49,032 ipo tayari kwa ajili ya kupandwa kwenye Halmashauri sita za Mkoa wa Kigoma” , alisema Kusaya.
Katibu Mkuu huyo amesema Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ( Mb) kesho Jumamosi anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku moja mkoani Kigoma kwa lengo la kugawa miche bora ya michikichi kwa wakulima na vikundi vya AMCOS .
Aidha,Waziri Mkuu Majaliwa atazindua rasmi zoezi la upandaji miche bora ya michikichi katika Gereza la Kwitanga na kambi ya JKT Bulombora.