Home Mchanganyiko RC MAKONDA ATOA SIKU 10 KWA MANISPAA YA KIGAMBONI KUHAKIKISHA HOSPITAL YA...

RC MAKONDA ATOA SIKU 10 KWA MANISPAA YA KIGAMBONI KUHAKIKISHA HOSPITAL YA WILAYA INAANZA KUTOA HUDUMA KWA WANANCHI.

0

******************************

Na Magreth Mbinga

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda ameutaka uongozi wa Manispaa ya Wilaya ya Kigamboni  kufikia June 1 mwaka huu hospitali ya Wilaya hiyo kuanza kutoa huduma rasmi.

Amezungumza hayo leo katika eneo la hospitali hiyo wakati alipoenda kukabidhi baadhi ya vifaa ambavyo ni magodoro,neti,shuka,ndoo,mopa,fagio na squezer pamoja na kukagua barabara ambayo inaendelea kujengwa katika Wilaya hiyo.

Aidha,Mh.Makonda amesema siku ya jumanne ya wiki ijayo atakabidhi mashine mbili za utrasound zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 70.

Pamoja na hayo Mh.Makonda amemtaka mganga mkuu wa Mkoa kutuma maombi wizarani ili kuhakikisha wanapatikana wafanyakazi 40 kwaajili ya kuanza kazi katika hospitali hiyo na ameahidi kutoa vitanda 120 kwaajili ya kuanzia.

Sanjari na hayo Mh.Makonda amemtaka Mkurugenzi wa TARURA ambaye anasimamia mradi huo wa barabara kujenga round about ambayo itakuwa kivutio kwa wote ambao watafika Kigamboni na iwe inatambulisha Wilaya hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mh. Sarah Msafiri amesema bado walikuwa wanapata changamoto wao kama ofisi ya Mkuu wa Wilaya waliona watoe baadhi ya vifaa katika ofisi zao ili kupunguza changamoto hospitalini hapo.

“Pamoja na changamoto hizo tulianza kutoa huduma ya mama na mtoto mpata sasa kaya zipatazo 32 zimepata huduma katika hospitali hii”amesema Sarah.