Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi akiangalia notis ya nyumba ambayo imeuzwa na shangazi wa watoto yatima Shamila Hussein na Omary Hussein bila wao kushirikishwa iliyopo jijini Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi akizungumza mara baada ya kuona jinsi nyumba ilivyouzwa kitapeli na Zakia Said ambaye ni shangazi ameuza nyumba ya watoto yatima ambao ni Shamila Hussein na Omary Hussein bila wao kushirikishwa iliyopo jijini Dodoma
Mtoto ambaye aliachiwa nyumba Shamila Hussein akieleza jinsi shangazi yao Zakia Said alivyowatapeli na kuiuza nyumba yao ambayo ni ya urithi kutoka kwa wazazi wao ambao wameshafariki imeuzwa bila wao kushirikishwa iliyopo jijini Dodoma
Mtoto ambaye aliachiwa nyumba Omary Hussein akieleza jinsi shangazi yao Zakia Said alivyowatapeli na kuiuza nyumba yao ambayo ni ya urithi kutoka kwa wazazi wao ambao wameshafariki imeuzwa bila wao kushirikishwa iliyopo jijini Dodoma
Mpangaji wa nyumba hiyo Bi.Mariam Shabani ambaye alipangishiwa na watoto Omary na Shamila Hussein akizungumza jinsi shangazi wa huyo aliyeamua kuuza nyumba kuwa yeye hamjui kwani ameanza kuishi na watoto tangu 2017 hivyo hajawahi kumuona ila anashangaa ameletewa notisi kuwa hatakiwi kukaa hapo.
Mjomba wa watoto hao Bw. Shamte Omary,akizungumza kuhusu shangazi yao ambaye sio mmiliki wa nyumba alivyoamua kuwatapeli kwa kuiuza hiyo nyumba bila kuwashirikisha na hana mamlaka yoyote kwa watoto Omary na Shamila wana hati ya kumiliki hiyo nyumba walioachiwa na wazazi wao.
jirani Mzee Ally Kassim,akitoa maeleza kuhusu marehemu Hussein alivyomuachia Hosia kabla ya Shangazi yao na Shamila na Omary Bi.Zakia Said kwenda kumuomba ili awe mrithi wa mirathi ya watoto.
Hii ndo nyumba ya watoto yatima Omary na Shamila ambayo imetapeliwa kwa kuuzwa na shangazi yao Bi.Zakia Said bila kuwashirikisha
…………………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi amewataka mawakili kutoleta masihala katika swala la haki za watanzania ili kutopoteza uchumi, Maisha na nguvu ya wanyonge katika nchi hii.
Kauli hii ameitoa Jijini Dodoma alipokwenda kuwaona Watoto yatima Shamila Hussein na Omary Hussein waliyotapeliwa na Shangazi yao nyumba yao ya kuishi.
Katambi amesema kuwa Serikali inawajibu mkubwa wa kusimamia sheria, taratibu na kanuni ikiwa ni Pamoja na maamuzi sahihi ya mahakama.
Katambi amesema kuwa notisi iliyotolewa ya kuwataka Watoto hao kutoka katika nyumba hiyo iliyouzwa ni batili hivyo wasiitekeleze na waendelee kuishi mpaka hapo atakapo wasiliana na mamlaka husika hasa mahakama ili kujua hatima na haki ya Watoto hao.
Hivyo Katambi amesema kuwa yeye kama mwakilishi wa Rais hapa Dodoma ataandika barua kwa mahakama ili kuhakikisha haki ya Watoto hao inapatikana kwani serikali ya awamu hii ya tano inajali wananchi wake ili waweze kutekeleza shughuli zao katika kuleta maendeleo yao na kukuza uchumi wa taifa.
Aidha Katambi amesema kuwa huyo shangazi yao Zakia Saidi Luguva ambaye ameuza nyumba hiyo awali aliitwa ofisini kwake hakutokea mpaka leo hivyo ameagiza vyombo vya ulinzi na salama kumfikisha katika ofisi yake popote atakapo kuwa akamatwe yeye na huyo mtu aliyenuna nyumba hiyo.
“Msimamizi wa mirathi uteuliwa na kikao cha ndugu wa uko na kuandika muhutasari ili kusikilizwa mahakamani ili kupitishwa au kupewa mamlaka hayo”, ameeleza Katambi.
Lakini Pia Katambi amebainisha kuwa msimamizi wa mirathi huwezi miliki mali hizo kwani msimamizi wa mirathi jukumu lake ni kugawa mali hizo kwa walengwa na kwa usawa.
Nao Watoto hao waliotapeliwa nyumba hiyo Shamila na Omary Hussein wamesema kuwa wamekuwa wakiishi katika nyumba hiyo tangu wazazi wao walipotangulia mbele za haki hawakuwahi kuona shangazi yao akiwasimamia wakiwa wadogo lakini hivi karibuni alijitokeza akidai husia kwa lengo la kutaka kuwa msimamizi wa mirathi .
“ Cha ajabu shangazi alikuja kutupa notisi hivi karibuni ya siku 14 akitutaka tutoke katika nyumba hii akidai ishauzwa hali ya kuwa sisi ni wahusika hatukupewa taarifa wala wapangaji wala majirani” wameeleza Shamila na Omary Hussein.
Watoto hao wameeleza kuwa shangazi yao Zakia Saidi Luguva akuwashirikisha katika hatua yoyote zaidi ya kuwatumia mesaji za vitisho za kuwataka kuwa watoka hapo ndani ya siku 14 kama notesi inavyowaelekeza Watoto hao.
Kwa upande wa Mjomba wao Shamte Omary ameeleza kuwa nyumba hiyo ilijengwa na wazazi wa Watoto hao kipindi wako hai na baadae waliitirafiana na kuachana ndipo baba yao aliandika husia wa kutaka nyumba na mali zote kurithiwa na Watoto wake aliyowazaa Marehemu Hussein.
“Watoto hawa wanahati ya nyumba hii cha hajabu huyo shangazi yao kaja na hati ambayo sisi kama ukoo na familia hatuitambui ndo kaitumia kuuza nyumba hii ya Watoto hawa.”, amebainisha Omary mjomba wa Watoto.
Naye jirani Mzee Ally Kassim amesema kuwa marehemu aliacha husia ukionyesha mmiliki wa mali zote kuwa ni Watoto wake lakini cha ajabu shangazi yao leo anawatapeli wakati katika husia huo hayupo alipoandikwa yeye kama shangazi wao.
Mwenyekiti wa Kisabudi ameeleza kuwa walikuja mawakili wakitaka asaini notesi ya kutaka kuwa toa Watoto hao akakataa ndo akaamua kuwaita Watoto na kuwauliza kama wanajua juu ya nyumba yao kuuzwa na kusema hawajui wala hawana taarifa zozote na kuwashauri kwenda mahakamani kudai haki yao.