Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akimkabidhi vifaa vya 85 vitakavyotumika kwa ajili ya usafi kwenye wilaya tatu zilizopo mkoani Tanga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ili viweze kusambazwa maeneo mbalimbali ikiwemo masokoni,hospitalini na stendi sambamba na kujenga masinki ya kunawia mikono kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari na Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Upendo Lugongo na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally halfa ya makabidhiano hayo ilifanyika mjini Pangani msaada huo ulitolewa na Tanga Uwasa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akimkabidhi vifaa vya 85 vitakavyotumika kwa ajili ya usafi kwenye wilaya tatu zilizopo mkoani Tanga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto ili viweze kusambazwa maeneo mbalimbali ikiwemo masokoni,hospitalini na stendi sambamba na kujenga masinki ya kunawia mikono kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Judica Omari na Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Upendo Lugongo na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Seif Ally halfa hiyo ilifanyika mjini Pangani msaada huo ulitolewa na Tanga Uwasa
Sehemu ya vifaa vilivyotolewa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly kulia akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makabidhiano hayo leo kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akinawa mikono na vifaa hivyo ambavyo vimetolewa na Tanga Uwasa kwa wilaya tatu mkoani Tanga wakati wa halfa ya makabidhiano leo kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) wametoa vifaa 85 kwa wilaya tatu zilizopo mkoani Tanga ili viweze kusambazwa maeneo mbalimbali ikiwemo masokoni,hospitalini na stendi sambamba na kujenga masinki ya kunawia mikono.
Vifaa hivyo vitagawiwa kwenye wilaya tatu ambazo ni wilaya ya Pangani, Muheza na Tanga ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha wanakabiliana na usafi wa kudumu kwenye maeneo mbalimbali
Akizungumza wakati akikabidhi vifaa hivyo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly alisema kwamba vifaa hivyo ni ndoo kumi kwa kila wilaya ambazo zitakuwa zimewekwa na koki kwa ajili ya kunawia vilivyotolewa na mamlaka hiyo.
“Kwa Pangani tumeleta ndoo 10 na Muheza ndoo 10 ambazo zitasambaza kwenye maeneo yaliyolengwa pia tutaendelea kujenga masinki ya kunaiwa kwa ajili ya usafi na sio Corona pekee yake “Alisema
Awali akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alisema kwa niaba ya ya Serikali ya Mkoa aliishukuru Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kwa kutoa msaada huo wa vifaa ambavyo vitatumika kwenye usafi wa kunawa mikono.
Alisema jambo hilo ni muhimu sana la kupambana na magonjwa mbalimbali na kwamba haulengi kwenye Corona kwa sababu tayari wamekwisha malizana nao huku akieleza kwamba msaada huo umefika wakati muafaka katika kuhakikisha jamii inanawa mikono na kujiweka kwenye hali ya usafi kila wakati.
“Msaada huu aulengi Corona kwa sababu tumekwisha malizana nalo una lenga kukabiliana na tatizo lolote hivyo nikuombe Mwenyekiti wa Halmashauri vifaa hivyo viwekwe kwenye maeneo yaliyokusudiwa na visiende kukwekwa kwenye stoo”Alisema RC Shigella.
“Lakini pia vifaa hivyo viwekwe kwenye maeneo ambayo watu wanaenda kunawa mikono kama sehemu ya utamaduni kila wakati na tuhakikishe tunanawa mikono kila wakati na huu uwe kama ustaarabu wetu”Alisema
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Pangani Seif Ally alisema kwamba wanaishukuruTanga Uwasa kwa msaada huo baada ya Mbunge wao Jumaa Aweso kupeleka ombi nao wakaona wamsaidie msaada huo ambao utawasaidia kupelekwa maeneo mbalimbali ili kusaidia usafi.
“Tanga uwasa walipewa ombi kuhusu suala hilo nao wakaona waweze kuja kutukabidhi leo lakini kubwa tuna mshukuru mbunge wetu Jumaa Aweso kwa kuwa mbunifu na kuweza kututafutia ndoo hizo “Alisema