MENEJA wa Benki ya CRDB Tawi la Zanzibar Ndg. Mbwana Ahmed akiwa amebeba mafuta ya kula wakati wa hafla ya kukabidha Vyakula mbambali kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar kwa ajili ya futari na maandalizi ya kusherehekea Sikukuu baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hafla hiyo imefanyika katika makaazi ya Watoto hao Mazizini Jijini Zanzibar.
MENEJA wa Benki ya CRDB Tawi la Zanzibar Ndg. Mbwana Ahmed akimkabidhi msaada wa Vyakula Mkuu wa Kituo cha Nyumba ya Watoto Yatima ya Mazizini Jijini Zanzibar.Bi.Pili Sadala, kwa ajili ya maandalizi ya Sikukuu ya Idd Il Fitry, hafla hiyo imefanyika katika Kituo hicho Mazizini na (kulia kwa Mkuu wa Kituo) Afisa Bima wa CRDB.Bi.Hamid Salim Juma na (kushoto kwa Meneja) Meneja Uhusiano na Serikali wa CRDB Ndg. Anasi Ramadhan. Hafla hiyo imefanyika katika jengo la kituo hicho mazizini.
MENEJA wa Benki ya CRDB Tawi la Zanzibar Ndg. Mbwana Ahmed akizungumza baada ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa ajili ya maandalizi ya Sikukuu baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa mtukufu wa Ramadhani kwa Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Jijini Zanzibar, kulia Mkuu wa Kituo cha Watoto Mazizini Bi. Pili Sadala na Afisa Bima wa CRDB.Bi.Hamida Salim Juma.
MKUU waKituo cha Watoto Yatima Mazizini Zanzibar.Bi. Pili Sadala akitowa shukrani kwa uongozi wa Benki ya CRDB Tawi la Zanzibar kwa msaada wao wa vyakulakwa ajili ya Watoto wa Kituo hicho na kutowa shukrani msaada huo umefika wakati muafaka, hafla hiyo imefanyika katika Kituo hicho Mazizini Jijini Zanzibar.(Picha na Othman Kondo)