Home Mchanganyiko TBL Plc KUTOA MSAADA VIFAA VYA KINGA YA COVID-19 KWA WATEJA WAKE...

TBL Plc KUTOA MSAADA VIFAA VYA KINGA YA COVID-19 KWA WATEJA WAKE KUPITIA MABAA ZAIDI YA 2,500 NCHINI

0

Meneja Mauzo wa TBL Plc, Silvanus Musomi (kulia) akimkabidhi Maneja wa bar ya Calabash     iliyopo Mwenge   jijini Dar es Salaam, Kiringa Wanzagi (wa pili kushoto) msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19, uliotolewa na kampuni   kwa ajili ya matumizi ya wahudumu na wateja ikiwa ni mwendelezo wa TBL kupambana na ugonjwa huo. Jumla ya baa 2,500 nchini kupatiwa msaada huo. wengine kwenye picha  ni  wafanyakazi wa baa hiyo   

Meneja Mauzo wa TBL  Plc,  Peter Mweta  ( wa pili kulia) akimkabidhi  Mmiliki  wa Bar ya  New Joint     iliyopo  External  Ubungo  jijini Dar es Salaam,  Olvari Shirima   (katikati) msaada wa  vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 uliotolewa na kampuni,  kwa ajili ya matumizi ya wahudumu na wateja  ikiwa ikiwa ni mwendelezo wa  TBL   kuunga mkono jitihada za  Serikali za kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo. Ma baa zaidi ya  2,500  nchini kupatiwa msaada huo , wengine kwenye picha  ni Afisa wa ukuzaji Masoko wa TBL, Neema Mkama  na wafanyakazi wa baa hiyo, Felista Patilio na Josephine Mshama.

……………………………………………………………………………………

Katika  jitihada zake za kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi yak ugonjwa wa  COVID 19,kampuni ya Tanzania Breweries Limited Company,(TBL Plc) imetoa msaada wa vifurushi vyenye vifaa vya kinga vyenye chupa ya vitakasa mikono na barakoa kwa ajili ya  wateja na wahudumu kwenye mabaa.

Akiongelea msaada  huo wa vifurushi  vyenye vifaa vya kinga ya COVID 19 ambavyo vitasambaza kwenye mabaa zaidi ya 2,500 nchini,Mkurugenzi Mkuu wa TBL Plc, Philip Redman, amesema   huu ni  mwendelezo  wa mchango wa kampuni katika kukabiliana na ugonjwa huu.

“ Kampuni ya TBL Plc inaamini  katika kujenga Dunia Maridhawa  katika uendeshaji wa biashara zake nchini,kupitia mchango huu inaungana na wateja wake na wadau wake wote katika kipindi hiki kigumu kwa kutoa mchango wa kukabili changamoto ya ugonjwa huu ili kuhakikisha tunakabiliana nao kwa pamoja”,alisema.

Katika siku za karibuni kampuni pia imetengeneza vitakasa mikono kwa ajili ya vituo vya afya nchini pote na kwa wadau mbalimbali ambao inashirikiana nao katika biashara zake.