Meneja Mauzo wa TBL Plc, Silvanus Musomi (kulia) akimkabidhi Maneja wa bar ya Calabash iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam, Kiringa Wanzagi (wa pili kushoto) msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19, uliotolewa na kampuni kwa ajili ya matumizi ya wahudumu na wateja ikiwa ni mwendelezo wa TBL kupambana na ugonjwa huo. Jumla ya baa 2,500 nchini kupatiwa msaada huo. wengine kwenye picha ni wafanyakazi wa baa hiyo
Meneja Mauzo wa TBL Plc, Peter Mweta ( wa pili kulia) akimkabidhi Mmiliki wa Bar ya New Joint iliyopo External Ubungo jijini Dar es Salaam, Olvari Shirima (katikati) msaada wa vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19 uliotolewa na kampuni, kwa ajili ya matumizi ya wahudumu na wateja ikiwa ikiwa ni mwendelezo wa TBL kuunga mkono jitihada za Serikali za kupambana na maambukizi ya ugonjwa huo. Ma baa zaidi ya 2,500 nchini kupatiwa msaada huo , wengine kwenye picha ni Afisa wa ukuzaji Masoko wa TBL, Neema Mkama na wafanyakazi wa baa hiyo, Felista Patilio na Josephine Mshama.
……………………………………………………………………………………
Katika jitihada zake za kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi yak ugonjwa wa COVID 19,kampuni ya Tanzania Breweries Limited Company,(TBL Plc) imetoa msaada wa vifurushi vyenye vifaa vya kinga vyenye chupa ya vitakasa mikono na barakoa kwa ajili ya wateja na wahudumu kwenye mabaa.
Akiongelea msaada huo wa vifurushi vyenye vifaa vya kinga ya COVID 19 ambavyo vitasambaza kwenye mabaa zaidi ya 2,500 nchini,Mkurugenzi Mkuu wa TBL Plc, Philip Redman, amesema huu ni mwendelezo wa mchango wa kampuni katika kukabiliana na ugonjwa huu.
“ Kampuni ya TBL Plc inaamini katika kujenga Dunia Maridhawa katika uendeshaji wa biashara zake nchini,kupitia mchango huu inaungana na wateja wake na wadau wake wote katika kipindi hiki kigumu kwa kutoa mchango wa kukabili changamoto ya ugonjwa huu ili kuhakikisha tunakabiliana nao kwa pamoja”,alisema.
Katika siku za karibuni kampuni pia imetengeneza vitakasa mikono kwa ajili ya vituo vya afya nchini pote na kwa wadau mbalimbali ambao inashirikiana nao katika biashara zake.