Viongozi wa dini wilayani Karagwe wakiwa kwenye
maandamano
Viongozi wa madhehebu ya Dini wilayani Karagwe wakimsikiliza mkuu wa wilaya baada ya kumaliza maandamano yao.
Asikofu Almachius Rweyongeza mwenye kanzu nyeupe pamoja na viongozi wengine wa dini wakiongea na viongozi wenzao wa dini.
Asikofu Almachius Rweyongeza kulia akiongea na
viongozi wenzake wa dini baada ya kupokea maandamano ya Amani yaliyolenga kumshukuru Rais Magufuli kwa kutofunga nyumba za ibaada na kuwaruhusu watanzania kuendelea kuabudu.
****************************
Karagwe
Na, Allawi Kaboyo,
Viongozi wa mathehebu mbalimbali ya dini wilayani Karagwe mkoani Kagera wamefanya maandamano ya Amani yenye lengo la kumshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kuruhusu kuendelea kufanyika kwa ibaada makanisani na misikitini kote nchini katika kipindi hiki cha mlipuko wa gonjwa hatali la COVID-19 linalosababishwa na virusi vya Corona.
Maandamano hayo yamefanyika leo yakitokea ofisi za mkuu wa wilaya hiyo na kupokelewa na mlezi wa kamati ya Amani ya wilaya hiyo Mwashamu Baba Askofu Almachius Vicent Rweyongeza wa jimbo la katoriki Kayanga pamoja na mkuu wa wilaya Mhe.Godfrey Muheruka katika viwanja vya nyumba ya vijana (ANGAZA) wilayani humo.
Kiongozi wa maandamano hayo mwenyekiti wa kamati ya maadili ya wilaya Karagwe Mchungaji Selesitin John wa kanisa la FPCT Kayanga amesema kuwa wameguswa na kauli ya Rais magufuli aliyoitoa mei 17 mwaka huu baada ya kushiri ibaada ya jumapili wilayani Chato.
Amesema kuwa suala la Rais Magufuli kuruhusu watanzania kuendelea kuabudu kwa kuliombea taifa na janga la Corona kwa kutofunga nyumba za ibaada linawapa msukumo mkubwa wa kuendelea kumshukuru na kumombea kwa mungu.
“Sisi viongozi wa dini wilayani Karagwe tunaungana na Rais Magufuli katika kipindi hiki cha Corona kuendelea kufanya ibaada huku tukichukua tahathali zote zinazotolewa na wataalamu wa afya, Magufuli alichaguliwa na mungu kuja kutuokoa sisi watanzania hivyo tunayo kila sababu ya kumuunga mkono na kuzidi kuliombe taifa letu libaki salama, niwaombe watanzania tuendelee kumuamini na kumuombea Rais wetu hili nalo litapita.” Amesema Mchungaji Selesitin.
Kwaupande wake Askofu Almachius baada ya kupokea maandamano hayo amewashukuru viongozi hao kwa mshikamano na umoja walioudumisha kwa maslahi ya wanakaragwe na watanzania kwa ujumla ambapo amesema kuwa kitendo cha kujitokeza hadharani na kumpongeza Rais Magufuli ni kitendo cha kizalendo nay eye kama mlezi wao amelipokea kwa nia njema.
Asikofu ameongeza kuwa nchi ya Tanzania ilimuhitaji mtu kama Rais magufuli ambaye mpaka sasa amekuwa mfano wa kuigwa kwa mataifa ya Africa na ulimwenguni kwa ujumla, na kuongeza kuwa kupitia maumbi na dua zinazoendelea kufanyika katika makanisa na misikiti katika kipindi hiki cha ugonjwa wa Covid-19 yamelifanya Taifa kuanza kuuepuka ugonjwa huu kama Rais alivyosema tunaendelea vizuri.
“Tumekuwa tukimsikia Rais Magufuli akituomba viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa na kuwasihi waumini wetu kufunga na kusali tukimuomba mungu wetu aweze kutunusuru na janga hili, sasa kupitia maombi na dua zetu mungu ameanza kutujibu ni wajibu wetu kama viongozi wa dini kudumisha Amani na mshikamano wetu bila kujali mathehebu yetu.” Asikofu Almachius amesema.
Asikofu amesisitiza kuwa wataendelea kuungana na Rais kwa kuwasihi waumini wao kufunga na kusali ili kumshukuru mungu kama Rais alivyotangaza siku tatu za maombezi ya shukurani yatakayofanyika kuanzia ijumaa ya tarehe 21 hadi jumapili ya tarehe 23 kwa makanisa yote wilayani humo.
Kwaupande wake Alhaji Sheikh Mustapha Muyonga Amiri wa wilaya Karagwe kutoka taasisi ya kiislamu JASUTA amesema kuwa licha ya kuwepo kwa janga la Corona waumini wa dini hiyo wameendelea kufanya ibaada mbalimbali ikiwemo kushiriki vipindi vya swala katika misikiti yao huku wakichukua tahadhali mbalimbali.
Amesema suala la Rais Magufuli kutofunga nyumba za ibaada limeliongezea daraja kubwa kwa mungu Taifa hili la Tanzania kwa uchamungu unaoendelea katika maeneo mbali mbali na kuongeza kuwa janga la Corona sio janga la kwanza Duniani maana yalikuwepo majanga mengi na makubwa kabla yetu.
“Kitendo cha Rais magufuli kuwaacha watanzania waendelee kuabudu ni kitendo cha kishujaa sana hivyo watanzania kwa imaani zetu tuendelee kumuombea Rais wetu na taifa letu, Kabla yetu yalikuwepo majanga tena makubwa lakini nyumba za ibaada hazikuwahi kufungwa hata nyakati za mitume, na mungu alishatwambia katika kitabu chake kitukufu Qur-an kuwa niombeni name nitawaitikieni hivyo tuzidi kumuomba na kumshukuru kila siku, sisi tumefunga na sasa tunaelekea kumaliza mfungo wetu wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na Inshaallah tutaswali na idd tukiwa salama. Amesema Alhaji Muyonga.
Mkuu wa wilaya Karagwe Godfrey Muheruka Baada ya kuwapokea viongozi wa dini amesema viongozi wa dini wilayani humo wamekuwa mfano wa kuigwa kwa kuhubiri Amani na mshikamano kwa wanakaragwe ambapo amewahakikishia Amani na usalama wakati wakiliombea taifa.
Muheruka amesema kuwa kuwa mbele kwa viongozi wa dini katika kuliombea taifa ni jambo la kizalendo kwa nchi yao na hilo ndilo analolihubiri Rais Magufuli kwa watanzania wote kuendelea kuomba na kusali ili tuweze kuepushwa na janga la Corona.
“Kwaniaba ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli mimi Godfrey Muheruka mkuu wa Wilaya ya Karagwe na wapokea viongozi wa dini waliojitokeza kufanya maandamano ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kuwaruhusu kuendelea kufanya ibaada katika nyumba za ibaada, niwahakikishi viongozi wangu wa dini sitawaangusha tutaendelea kuwa pamoja katika mapambano dhidi ya Corona.”
Mkuu huyo ameongeza kuwa wananchi kupitia viongozi wa dini wandelee kufanya ibaada huku wakifuata taratibu zote zinazotolewa na wataalamu wa afya katika maeneo mbalimbali na kuongeza kuwa Corona ipo lakini wanatakiwa kutokuwa na hufu huku akisistiza kuendelea kufanya kazi kwa kulijenga taifa lao.
“Mimi niseme tu wapo baadhi ya viongozi walitangaza kufunga makanisa hapa wilayani suala lililowapelekea wananchi kutishia kulichoma kanisa hilo, lakini tulivyoona hali hiyo tulijitahidi kuizui hali hiyo na kanisa halikuchomwa, hivyo nitoe wito kwa viongozi wa dini waacheni waumini wenu wafanye ibaada maana gonjwa hili ni gonjwa kama magonjwa mengine na sio kila anayeumwa anaumwa Corona, niwahakikishieni kwa wilaya Kargwe mpaka sasa tupo salama hatuna mshukiwa wala mgonjwa wa Corona tuendeleeni kuomba na kufanya kazi.” Amesema Muheruka.
Viongozi hao wamesema kuwa wataungana na watanzania wote pamoja na Rais Magufuli katika kufanya ibaada ya Shukrani kwa mungu kwa ambayo itadumu kwa siku tatu kama Rais Magufuli alivyotangaza kwa lengo la kumshukuru mungu kwa namna anavyolibariki taifa la Tanzania