Mkuu wa kitengo cha rasilimaliwatu Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Anthony Rutashuburugukwa, akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Maabara wa Hospitali ya Polisi Kilwa Road wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kitabibu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170 vilivyotolewa na Ushirika wa Kuweka na
Kukopa Fedha wa Usalama wa Raia (URA SACCOS) kwa ajili ya hospitali hiyo. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa kitengo cha rasilimaliwatu Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Anthony Rutashuburugukwa, akikata utepe kuashiria kupokea vifaa vya kitabibu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170 kutoka Ushirika wa Kuweka na Kukopa Fedha wa Usalama wa Raia (URA SACCOS), kulia kwake ni mwakilishi wa bodi ya URA SACCOS, Stanford Busumbiro na kushoto kwake ni
Kamanda wa Kikosi cha Afya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hussein Yahaya. (Picha na Jeshi la Polisi)
Mkuu wa kitengo cha rasilimaliwatu Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Anthony Rutashuburugukwa, akikagua vifaa vya kitabibu katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road, vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 170 vimetolewa na Ushirika wa Kuweka na Kukopa Fedha wa Usalama wa Raia (URA SACCOS) kwa ajili ya hospitali za Polisi Tanzania, kulia kwake ni mwakilishi
wa bodi ya URA SACCOS, Stanford Busumbiro na kushoto kwake ni Kamanda wa Kikosi cha Afya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Hussein Yahaya. (Picha na Jeshi la Polisi).