Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (wa pili kulia) akiwa katika ziara ya kutembelea kiwanda cha kutengeneza chokaa cha Neelkanth cha jijini Tanga kukagua utekelezaji wa sheria ya mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima akiangalia mojawapo ya mawe yanayotumika kutengenezea chokaa katika kiwanda cha Neelkanth cha jijini Tanga ambacho kinalalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kufikiwa na vumbi.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (wa pili kulia) akiwa katika ziara ya kutembelea kiwanda cha kutemgeneza chokaa cha Neelkanth cha jijini Tanga kukagua utekelezaji wa sheria ya mazingira.
Ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (wa pili kulia) ikiendelea katika kiwanda cha kutemgeneza chokaa cha Neelkanth cha jijini Tanga.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima (wan ne kulia) akisikiliza taarifa kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella mara baada ya kuwasili mkoani humo kuanza ziara ya kikazi.
………………………………………………………………………………………….
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Sima amemuelekeza mwekezaji wa kiwanda cha chokaa cha Neelkanth Chemical cha jijini Tanga kubuni njia mbadala ya kuzuia vumbi kutoka na kusambaa hewani hivyo kuleta athari kwa wananchi.
Sima alitoa agizo hilo jana alipofanya ziara ya kukagua kiwanda hicho ambapo pamoja na mambo mengine ililenga kumpa maelekezo ya namna ya kuendesha shughuli bila kuathiri mazingira.
Alibainisha kuwa mashine zilizopo hapo hazina uwezo wa kuzuia vumbi kusambaa jambo ambalo ni hatari kwa afya ya wafanyakazi na wananchi wakati moshi unapofuka hewani.
Alilielekeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wapime na waangalie ni madhara gani ya kiafya kwani unakwenda kwenye makazi ya watu.
“Mazingira ya kiwandani hapa ni ya kawaida lakini tunashuhudia moshi na vumbi vikisambaa ni sawa wana consultant (mshauri) hapa standards (viwango) zinatofautiana hivyo ndio maana nimeelekeza NEMC wapime washauri nini kifanyike,” alisema.
Aidha, Naibu Waziri Sima alisisitiza kuwa pamoja na Serikali kualika wadau kuwekeza katika sekta ya viwanda lakini pia inao wajibu wa kuhakikisha viwanda vinafanya shughuli zake bila kuathiri mazingira na wananchi wanaozunguka.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Ndimbumi Yoram alisema kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi kuhusu vumbi na moshi vinatoka kiwandani hapo.
Alitoa mwito kwa mwekezaji huyo ambaye pamoja na kujikagua na kutoa ripoti kwa Baraza hilo lakini pia awaruhusu kufanya ukaguzi wakati mashine zinafanya kazi ili waweze kushauri.
“Tunaona vumbi kwenye ambalo limetokana na kusaga mawe haya ya kutengenezea chokaa lakini kwa sababu mitambo imezimwa hatuwezi kujua linatoka wapi hivyo mwenye kiwanda awe muwazi aturuhusu tukague kikiwa kinafanya kazi ili tujue vumbi linatoka wapi na tuweze kumshauri,” alisema Ndimbumi.
Nae Mkurugenzi wa kiwanda hicho Rashid Hamoud aliishukuru Serikali kupitia kwa Naibu Waziri huyo kwa kutembelea na kuahidi kutekeleza maelekezo yote yaliyotolewa.