Mhe. Andrew Massawe, katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, wa kwanza kushoto akisisitiza jambo alipotembelea utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda cha bidhaa za ngozi cha Karanga kilichopo Kilimanjaro
Engineer Masoud Omari akifafanua jambo wa pili kulia akifafanua jambo kwa katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu,
Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF Bw. Hosea Kashimba wa kwanza kushoto akifafanua jambo kwa katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu,
***********************************
Ofisi ya Waziri mkuu Imeziagiza Jeshi la Magereza nchini na Mfuko wa hifadhi ya Jamii PSSSF,zinazotekeleza kwa pamoja mradi wa zaidi ya shilingi bilioni 75 wa kiwanda cha bidhaa za ngozi eneo la Karanga,Moshi,Mkoani Kilimanjaro,ambao umefikia asilimia 95 kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati miundombinu ambayo bado
kukamilika ili kiwanda kianze uzalishaji mara moja.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, ANDREW
MASSAWE,ametembelea mradi huo na kutoa maagizo matatu kwa pande mbili zinazotekeleza mradi huo ikiwemo kuhakikisha vifaa vya umeme vilivyoagizwa kwa kampuni za ndani vinapatikana na mkazo mwingine kuhusiana na ulinzi hususani wa mashine ambazo tayari zimeshawasili kufutia gharama yake kubwa.
Katika Hatua nyingine wakuu wa Taasisi wabia katika mradi huo,wametoa mitazamoa yao kufuatia maagizo ya Ofisi ya waziri mkuu.
Matarajio ya kiwanda hicho cha kimkakati ambacho ni upanuzi wa kiwanda cha sasa kinachozalisha jozi 400 za viatu kwa siku,zikiwemo buti za jeshi na kiraia,ni ,kuzalisha jozi 4,000 za viatu vya kiraia pekee kwa siku sawa na takribani jozi milioni 1.2 kwa mwaka kikiratajiwa kuzalisha jumla ya ajira 7,000