Kampuni ya simu za mkononi ya TECNO imebainishwa kuwa ndio kinara kwa Tanzania katika mauzo ya simu yake mpya ya TECNO CAMON 15 huku ikiwa na muda wa mwezi mmoja tu tangu izinduliwe na kuingizwa sokoni rasmi.
TECNO CAMON 15
Akizungumza na mwandishi wetu aliyetaka kujua mwenendo wa soko la vifaa vya kielektroniki hasa kipindi hiki cha janga la ugonjwa wa COVID-19 leo jijini Dar es Salaam, meneja mauzo wa kampuni ya simu ya TECNO Bi. Mariam Mohamed ameeleza kuwa ubora wa TECNO CAMON 15 na uzingatiaji wa mahitaji ya wateja wao ndivyo vitu vilivyofanya simu hiyo kuuzwa sana ndani ya mwezi mmoja.
“Tumezindua CAMON 15 katikati ya mwezi Aprili mwaka huu lakini mpaka sasa tumeweza kuuza CAMON 15 pisi zaidi ya 2500 huku kukiwa bado kuna hitaji kubwa la wateja” Alisema Bi. Mariam.
Bi. Mariam aliongeza kuwa, “TECNO tumeaminiwa sana na wateja na sababu kubwa ya kuongoza kimauzo ndani ya mwezi mmoja ni kutokana na ubora wa CAMON 15 ambayo ni simu iliyozingatia soko la sasa na mahitaji ya teknolojia ya kisasa kwa wateja wetu.”
Meneja Mauzo wa kampuni ya TECNO Bi. Mariam Mohamed akiwa katika moja ya duka kubwa la TECNO jijini Dar es Salaam TECNO CAMON 15 inayosifika kwa kamera yake,betri, mwonekano na skrini yake. Simu hiyo ina kamera tatu nyuma lensi na flash ambapo kamera kuu ina MP64 huku kamera ya mbele ikiwa na MP32.
Ikumbukwe kuwa TECNO CAMON 15 ilizinduliwa katikati ya mwezi Aprili kwa njia ya mtandao huku msanii maarufu wa bongo muvi Elizabeth Michael (LULU) akitambulishwa kama balozi wake.
Balozi wa TECNO CAMON 15 Bi. Elizabeth Michael (LULU) akiwa na mchekeshaji maarufu Jaymond katikati ya mwezi Aprili mara baada ya kuzindua CAMON 15.