…………………………………………………………………………….
Silvia Mchuruza,Bukoba
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya bukoba vijijini mkoani kagera mh. Murshid Ngeze amezipongeza juhudi za serikali ya mkoa na serikali kuu kwa ujumla kufuatia ujenzi wa chuo kikubwa cha mafunzo ya ufundi stadi veta kinachojengwa na shanxi construction investment group campany limited ya nchini china kilichowekwa jiwe la msingi na waziri wa elimu mwaka jana professa Joice Ndalichako kutokana na chuo hicho kuwa na uwezo wa kudaili wanafunzi 800 wa kozi ndefu na 1000 wa kozi fupi kitakapo kamilika.
Akizungumza wakati alipokuwa akifanya ukaguzi wa mradi wa chuo hicho ambapo aliongozana na kamati ya fedha ya halmashauli hiyo amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi wa kata nyakato na hata mkoa mzima wa kagera watanufaika zaidi kutokana na mradi huo ukikamilika ambapo unategemea kukamilika baada ya miezi 18 na utaghalimu fedha za kitanzania shilingi bilioni 22.04.
“naamini wananchi wa kijiji cha burugo kata ya nyakato watanufaika sana lakini pia nakumbuka wanachi hawa waliahaidiwa maji ya huakika na umeme kupitia mpango wa kupeleka umeme vijijini REA basi mimi nitakumbusga mamlaka husika kuhakikisha wanachi hawa wanapata umeme na maji ya kutosha kutokana na kujitoa bure bila gharama zozozte katika eneo hili la ujenzi wa chuo eneo lenye ukubwa wa hekta 40.58”
Aidha nae msimamizi wa mradi huo Bwn.Ally Bushiri ambae ni muwakilishi wa mkuu wa chuo katika mradi amesema kuwa hadi sasa ujenzi wa chuo hicho unaendelea vizuri kwa kushirikiana na serikali ya china na tanzania na kuipongeza serikali ya mkoa kwa ufuatiliaji mzuri katika ujenzi wa chuo hicho mpaka sasa.
Hata hivyo licha ya maendeleo mazuri ya mradi huo amezitaja changamoto wanazokumbana nazo katika ujenzi huo ikiwemo ukosefu wa maji ya kutosha lakini pia ukosefu wa mtandao mzuri kwa ajili ya mawasiliano kwa wafanyakazi wote kutokana na jiografia ya mkoa wa kagera ilivyo.
“tunaendelea vizuri lakini kama mnavyojua jiografia ya mkoa wetu ilivyo maeneo haya mtandao sio mzuri ukizingatia hapa watakuja wanafunzai wengi sana na wao watakuwa wanatumia mtandao tunaiomba serikali kuwekea mkozo hili zaidi ili kuweza kutusaidia hasa sisi wenyewe tuliopo katika mradi huu ili kuweza kufanya kazi kwa weredi japo kwa sasa kazi aziendi vizuri kutokana na uwepo wa ugonjwa wa corona kuathiri zaidi maeneo yaliyo mengi duniani hivyo kumzuia mkandalasi kuagiza mafundi wengine kutoka nchini china”