Home Mchanganyiko WAZIRI MKUU AFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI MRADI MKUBWA WA UMEME WA...

WAZIRI MKUU AFURAHISHWA NA KASI YA UJENZI MRADI MKUBWA WA UMEME WA JULIUS NYERERE WA MW 2115

0

WAZIRI
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Kassim Majaliwa ameridhishwa na hatua
mbalimbali za ujenzi wa Mradi mkubwa wa Kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere
(JNHPP) unaotekelezwa kwenye mto Rufiji.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo Mei 14, 2020, baada ya kufanya ziara kwenye eneo la
mradi unaotarajiwa kuzalisha jumla ya Megawati 2115“ utakapokamilika 2022.
Waziri
Mkuu ambaye alifuatana na Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo mhandisi Zena Said watendaji wa TANESCO wakiongozwa na
Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dk.Tito Mwinuka, alisema ziara yake ililenga
kupata picha halisi ya hali ya mradi na hatua iliyofikiwa.
“Nimefarijika
sana kuona hatua iliyofikiwa toka mradi umeanza mwezi Juni mwaka Jana mpaka leo
ni ya kuridhisha.” Alisema Waziri Mkuu.
Alisema
ziara yake imempa fursa ya kujionea jinsi kazi zinavyoendelea na nimatumaini
yake
utakamilika
kwa wakati
“Nimepata
fursa ya kuona eneo lote la mradi na kazi mbalimbali zikiendelea, wakandarasi
wanafanya vizuri na sisi Kama Serikali kupitia Wizara na TANESCO tumekuwa
karibu nao kuhakikisha wanafanya vizuri na hayo ndio matarajio ya watanzania.”
alisema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu amewahakikishia watanzania kuwa mradi huo utakamilika katika muda
uliopangwa na kuwapongeza wakandarasi kampuni ya Elsewedy na Arab contractor
kutoka Misri kwa kazi nzuri.
Alisema
licha ya changamoto ya mvua za masika bado kazi ya ujenzi iliendelea.
Awali
akitoa taarifa ya utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo Waziri wa Nishati Dkt.
Medard Kalemani alisema, ujenzi ulianza 15/6/2020 na utakamilika 14/6/2022.
“Mradi
unashughuli kubwa saba kati ya hizo muhimu sana ni nne, ujenzi wa njia ya
kuchepusha maji, kujenga bwawa lenyewe, kujenga kingo nne zitakazowezesha maji
kuhifadhiwa na ya mwisho ni kujenga power house.”. alifafanua Dkt. Kalemani.
Dkt.Kalemani
alisema Hadi sasa mkandarasi ameshalipwa shilingi trilioni 1.29 ya jumla ya
shilingi trilioni 6.5 ya mkataba mzima. “Malipo hayo ni sawa na asilimia 100 ambayo
inahusu malipo ya awali asilimia 15 na malipo ya kazi alizofanya Hadi sasa.”
Alifafanua Dkt. Kalemani.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akiwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akizungumza wakati alipotembeela eneo la ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) wa MW 2115 huko Rufiji Mkoani Pwani Mei 14, 2020.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama maendeleo ya  ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere kwenye mto Rufiji mkoani Pwani Mei 14, 2020.

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati, mstari wa mbele) akiongozana na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said (kulia) wakati akitembeela ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye mto Rufiji mkoani Pwani, Mei 14, 2020
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO (Anayeshughulikia Miundombinu na Uwekezaji) Mhandisi Khalid James), akiteta mwakilishi wa kampuni iliyopewa kandarasi ya ujenzi wa mradi wa JNHPP ya El Sewedy Electric kutoka Misri.
 Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara hiyo.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kulia) mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa majai wa Julius Nyerere (JNHPP) kwenye bonde la mto Rufiji mkoani Pwani Alhamisi 14/5/2020.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia) akizungumza na wakandarasi wanaotekeleza ujenzi wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere, Arab Contractors na Elsewedy kutoka nchini Misri, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo utakaozalisha MW 2115 za umeme. Waziri  Mkuu alitembeela mradi huo Alhamisi 14/5/2020.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wakwanza kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi qa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (aliyevaa nguo nyeusi), Katibu Mkuu Wizara ya Nishatio Mhandisi Aziza Said (wapili kushoto) na wakandarasi wa kampuni za Arab Contractors na Elsewedy zote kutoka Misri, wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kutembelea mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) huko Rufiji Mkoani Pwani 14/5/2020.
 Taswira ya baadhi ya maeneo ya ujenzi wa mradi wa JNHPP leo Mei 14, 2020
 Taswira ya baadhi ya maeneo ya ujenzi wa mradi wa JNHPP leo Mei 14, 2020