*********************************
Na Magreth Mbinga
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva na mjasiriamali Zuwena Mohammed ‘Shilole’ na Mtangazaji wa Clouds Masoud Kipanya wamepewa Ubalozi wa kampeni mpya ya ‘Naweza’ inayosimamiwa na Smart Generation ili kutoa mafunzo ya elimu ya uzazi.
Wakizungumza na waandishi wa habari, Smart Generation iliyo inayoongozwa na Mtangazaji wa CloudsFm Ciza pamoja na Msanii wa Bongo fleva anayetokea katika kundi la Weusi Nickso Nikkiwapili.
“Wanawake tusimame imara kwa ajili ya watoto wetu, wanaume hawawezi, mimi naweza kweli ndio maana nimeisimamia familia yangu, nikisema nataka kupata mimba ya Uchebe nitaenda Clinic mapema, kuna faida ya kuwahi Clinic”alisema Shilole baada ya kutambulishwa kuwa balozi.
Pia Masoud Kipanya baada ya kupewa Ubalozi aliongea haya “Msindikize Mama clinic, mbali na hilo, wanaume tunatakiwa tuache nafasi ya kutompa mkeo ujauzito kati ya mimba na mimba, kipindi hiki ambacho kuna corona, muda mwingi tupo nyumbani,”
“Nadhani wanaume mnanielewa, tupangilie uzazi lakini pia tuwe mstari wa mbele kuhakikisha malezi ya mtoto yatakuwa ya wote kati yako na mwenza wako, tusiwaachie akina mama pekeyao maana mtoto sio wa kwao peke yao bali mtoto ni wa wote mume na mke”alisema Masoud