*********************************
Magreth Mbinga
Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam wametakiwa kudai risiti pindi wanaponunua sukari kwa bei ya rajaraja ili kuweza kuwabaini wale wote ambao wanauza bei tofauti na bei ambayo tofauti na iliyotolewa na serikali.
Amezungumza hayo mkuu wa mkoa wa Dar es salaam My Paul Makonda wakati wa kukabidhiwa gari na kampuni ya TATA kwaajili ya kubebea wahudumu wa afya wa mkoa .
Pia Makonda amesema mfuko mmoja wa sukari wa kg 50 unauzwa shilingi 115,000 hivyo wauzaji wasiwauzie wanunuzi wa rejareja bei tofauti na iliyoelekezwa na serikali ambayo ni 2600.
Vilevile Makonda amesema hali ya mkoa inaendelea vizuri kutokana na watu kuendelea kuchukua hatua ya kupambana na Corona kwa kuvaa barakoa,kunawa mikono na kuzingatia umbali wa Mira moja baina ya watu.
“Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam muendelee kufanya mazoezi ili kujilinda na magonjwa mengine kama vile kisukari na yanayotokana na kutokufanya mazoezi” amesema Makonda.
Sanjari na hayo Makonda amewataka wananchi wa mkoa huo kupuuzia taarifa zinazotolewa na waovu na wizara haina sababu ya kuficha ukweli kama halo itakuwa mbaya waendelee kuchukua tahadhari huku wakiendelea kufanya kazi.
Hatahivyo Makonda amewashukuru kampuni ya TATA kwa ushirikiano ambao wameuonesha kwa juhudi za kupambana na ugonjwa huu wa Corona kwa kutoa gari ya kubebea wahudumu wa afya.