Akina mama Wilayani Nyasa wakimshukuru mbunge wa Nyasa Mhandisi Stela Manyanya kwa kuwakabidhi gari ya kubebea wagonjwa katika kituo cha afya Mbamba-bay, Wilayani Nyasa, keroiliyokuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu.Gari imetolewa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kwa utamaduni wa kabila la Wanyasa Kulala chini ni kushukuru kupita kiasi.(Picha na Ofisi ya Mkurugenzi Nyasa)
…………………………………………………………………………………..
Akina mama wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma wamesema wamepata hamu ya kuzaa, baada ya kukabidhiwa rasmi Gari ya kubebea wagonjwa ya Kituo cha afya Mbamba-bay.
Gari hiyo imekabidhiwa jana katika Kituo cha afya cha Mbamba-bay Wilayani hapa na Mbunge wa Jimbo la Nyasa Mhandisi Stela Manyanya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na kupokelewa na Uongozi wa Kituo cha afya Mbamba-bay Wilayani hapa.
Akinamama hao walimueleza mbunge kuwa ,Hamu ya kuzaa imeongezeka kutokana na kupewa gari mpya ya kubebea wagonjwa, kwa kuwa mwanzo walikuwa wakikumbana na adha ya Uzazi pale wanaposhindwa kujifungua na kulazimika kupata gharama nzito ya kukodi gari ili kwenda, Hospitali kubwa kwa uchunguzi zaidi.lakini kwa sasa, hawana tena wasiwasi kwa kuwa gari ipo.
“Tunaishukuru sana Serikali ya Rais John pombe magufuli, na mbunge wetu wa Nyasa kwa kutuletea gari ya Wagonjwa katika kituo chetu cha afya cha Mbamba-bay, Awali tulikuwa hatuna hamu ya kuzaa kwa kuwa tulikuwa tukuhofia usalama wetu wa afya ya uzazi kama tulikuwa tukipata matatizo ya Uzazi kulikuwa hakuna usafiri wa uhakika wa kutufikisha hospitali kubwa lakini kwa sasa Hamu ya kuzaa imeongezeka kutokana na kukabidhiwa gari jipya ambalo tumekabidhiwa leo”.alisema mariana Kapinga
Awali akitoa Taarifa fupi ya Kituo cha Afya kwa Mgeni Rasmi Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Mbamba-bay Michael Mabisi alisema Kituo hicho kwa sasa kinaendelea vizuri na changamoto nyingi za vifaa tiba na vitendea kazi viko katika Hali nzuri na kumpongeza Mh. Mbunge kwa mchango mkubwa wa kukiboresha Kituo cha Afya cha Mbamba-bay na Wilaya ya Nyasa kwa ujumla wake.
“Mh Mbunge sisi wafanyakazi wa kituo cha Afya Mbamba-bay tunatambua mchango wako wa hali na mali wa kuboresha sekta ya Afya, Hususani kuboresha Kituo hiki kwa kutatua changamoto nyingi zilizokuwa inakikabili na Leo hii umetukabidhi gari la Wagojwa tunakushukuru sana.Kama wafanyakazi tunatembea kifua mbele kwa kwa tuna Mbunge anayejali Watumishi, anayejali afya ya Jamii”Alisema Dkt Mabisi.
Akikabidhi Gari ya Wagojwa Mbunge wa Nyasa Mhandisi Stela Manyanya, Alisema anamshukuru Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe magufuli kwa kuwajali wananchi wa Nyasa , kwa kutupa miradi mbalimbali ya Afya kwa kuwa tumejengewa Hospitali ya Wilaya na Vituo vya afya vya Mkili, Kihagara, Kingerikiti na Kuboresha Miundombinu ya Vifaa tiba ,na Miradi mingine mingi ya Maendeleo kwa Wilaya ya Nyasa.Inaonyesha ni jinsi gani anatupenda Wananyasa na leo hii ametupatia gari ya Wagonjwa mpya ambayo itasaidia kubeba wagonjwa na shughuli zingine za Afya.
Amewataka Uongozi wa Afya kituoni hapo kulitunza gari hilo ili liweze kuwa zima muda wote kwa kuwa gari ni mali ya Wananchi na Dereva atakayepata alitunze atembeze kwa uangalifu na kutunza Siri za akina mama hao.