Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Emanuel
Ndomba kulia akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira ya bahari Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigella leo vyenye thamani ya sh.milioni 70 walivyovitoa kwa kushirikiana
na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira ya Bahari (Marine Parks and Reserves
Tanzania) kushoto ni Mhifadhi Ufundi,Ununuzi na Ufuatiliaji wa Hifadhi za
Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania Clever Charles Mwaikambo
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Emanuel
Ndomba kulia akimkabidhi vifaa vya usafi wa mazingira ya bahari Mkuu wa Mkoa wa
Tanga Martine Shigella leo vyenye thamani ya sh.milioni 70 walivyovitoa kwa kushirikiana
na Shirika la Uhifadhi wa Mazingira ya Bahari (Marine Parks and Reserves
Tanzania) kushoto ni Mhifadhi Ufundi,Ununuzi na Ufuatiliaji wa Hifadhi za
Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania Clever Charles Mwaikambo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Emanuel
Ndomba
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Emanuel
Ndomba akizungumza kabla ya makabidhiano hayo kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Emanuel
Ndomba katikati akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella
MKUU wa Mkoa wa Tanga akisanitizer kabla ya kufanya makabidhiano hayo ambaye
anamueweka kwenye mkono ni Afisa Habari wa TASAC Nicholous Kinyariri
SEHEMU ya vifaa hivyo
*********************************
MKUU wa Mkoa wa Tanga,Martin Shigella leo amekabidhiwa vifaa vya usafi wa mazingira ya bahari vyenye thamani ya shilingi milioni 70 vilivyotolewa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania(TASAC) pamoja na Shirika la Uhifadhi Mazingira ya Bahari(Marine Parks and Reserves Tanzania).
Vifaa hivyo ni kwa ajili ya kusafisha mazingira ya bahari yaliyochafuliwa na mafuta ghafi.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi Mkuu wa TASAC,Emmanuel Ndomba amesema kuwa vifaa hivyo ni vya aina mbili na ni vya huduma ya kwanza vya kudhibiti uchafuzi wa mazingira ya bahari unaosababishwa na kumwagika kwa mafuta.
Alivitaja vifaa hivyo kuwa ni kifaa cha kuwezesha vifaa vingine kinachoitwa ‘power parks’ ambacho kinaendesha vifaa vya kutenganisha maji na mafuta kinachoitwa ‘skeamer’ na kifaa cha kusukumia maji.
Amesema kuwa TASAC na Shirika la Uhifadhi Mazingira ya Bahari kwa pamoja wametoa vifaa hivyo kwa malengo makuu matatu ambayo ni kuunga mkono juhudi za serikali katika kupambana na uchafuzi wa mazingira ya bahari,kujenga uchumi wa nchi kwa watu wanaoishi katika mazingira ya bahari na kusaidia mafunzo ya usafi wa mafuta yanayomwagika baharini kwa wadau wa mazingira ya bahari.
” Sisi TASAC kwa kushirikiana na wenzetu wa Marine Parks tumeamua kuunga mkono juhudi za serikali katika kutunza mazingira ya bahari,”alisema.
Kwa upande wake,Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela amewashukuru TASAC na Marine Parks kwa msaada huo na kusema kuwa umekuja wakati muafaka haswa katika bandari ya Tanga haswa katika kipindi hiki ambacho bandari hiyo ipo kwenye upanuzi na pamoja ujio wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda.
Amesema kuwa vifaa hivyo ni matokeo ya ahadi iliyotololewa mwezi Septemba mwaka jana wakati wa mafunzo ya usafi wa mazingira ya bahari yaliyotolewa na TASAC .
Amesema kuwa vifaa hivyo vitapatikana kwa muda wa saa 24 ndani ya siku saba za wiki pindi mafuta yatakapomwagika iwe rahisi kuyaondoa kwa wakati.
Aidha,amewataka watumishi na wadau wa wote wa bahari kutimiza wajibu wao na kutaka ikiwezekana kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya usafi wa mazingira ya bahari.
Kuhusu upanuzi wa bandari ya Tanga, Shigella alisema kuwa tayari mashine ya kuchimba kina cha bahari umemaliza kazi yake kinachofuata ni kuletwa kwa vifaa kwa ajili ya ujenzi wa gati