Waziri wa Nishati Mhe Medard Kalemani akiteta jambo na
Naibu Mkurugenzi mtendaji shirika la umeme Tanzania(TANESCO) Khalid Jems, wakati alipofanya azira ya kukagua ujenzi wa msongo wa umeme kwa ajili ya reli ya kisasa (SGR) Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nishati Mhe Medard Kalemani akipewa maelezo ya Kiwanda na mmoja wa Viongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, alipofanya ziara ya siku moja kiwandani hapo ili kukagua miondombinu ya umeme.
03.Waziri wa Nishati Mhe Medard Kalemani akitoa maelekezo kwa Naibu Mkurugenzi mtendaji shirika la umeme Tanzania(TANESCO) Khalid Jems,alipofanya ziara ya siku moja ya kukagua ujenzi wa msongo wa umeme kwa ajili ya reli ya kisasa (SGR), Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nishati Mhe Medard Kalemani akiongea na
wananchi ambao maeneo yao yamepitiwa na mradi ya msongo wa umeme, Mkoani Morogoro.
Waziri wa Nishati Mhe Medard Kalemani akikagua moja ya
mtambo wa umeme uliopo katika kiwanda cha sukari cha Mtibwa. Mkoani Morogoro.
*******************************
NA FARIDA SAIDY MOROGORO
Ili kuimarisha viwanda vilivyopo hapa nchini na kufikia adhima ya serikali ya awamu ya tano ya Tanzania ya viwanda inayoongozwa na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jonh Pombe Joseph Magufuli,Serikali kupitia Wizara ya Nishati imetenga shilingi Bilioni
1.2 kwa ajili ya kujenga njia za kupitishia umeme kwenda kiwanda cha sukari cha mtibwa kilichopo mkoani morogoro.
Mhe kalemani amesema ili kumaliza changamoto za kukatika kwa umeme mara kwa mara katika kiwanda hicho ambazo zimekuwa zinawasumbua kwa muda mrefu ni lazima kuachanisha njia za umeme kati ya kiwanda na wananchi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati Mhe Medard Kalemani alipofanya ziara katika kiwanda cha sukari cha mtibwa ,na njia maalumu za umeme kwa ajili ya reli ya kisasa (SGR) awamu ya kwanza kutoka Dar es salaam hadi morogoro km 161.
Aidha waziri kalemani ametaja sababu zinazosababisha kiwanda hicho kukosa umeme wa uhakika kuwa ni pamoja na umbali, kwani kiwanda kinapokea umeme kutoka msamvu,ambapo umeme huo pia unagawanywa kwenye vijiji mbalimbali jambo linalosababisha kiwanda kupata umeme mdogo.
Alisema Sababu nyingine ni miundombuno inayopeleka umeme katika kiwanda hicho kuwa chakavu,kwani ilianza kutumika toka mwaka 1965 yaani tangu kiwanda hicho kilipofunguliwa.
Awali akiongea kwa niaba ya uongozi wa kiwanda cha Sukari cha Mtibwa Mhandisi Juma Palamba amemuomba Waziri Kalemani kuwaongezea umeme ili waweze kuzarisha sukari kwa wingi na kuwaondolea adha wananchi ya kuatafuta sukari hususani katika kipindi
cha ramadhani.
Awali akiwa katika eneo la ujenzi wa msongo wa umeme, maalumu kwa ajili ya Reli ya kisasa (SGR), Waziri Kalemani amemtaka makandarasi kumaliza kazi ndani ya muda uliopangwa,kwani amebakiza siku chache mkataba wake kuisha,ambapo mwisho wa mkataba huo ni mwezi May, 2020.
Kwa upande wake mkandarasi anayejenga mardi huo wa njia za umeme amemuhakikishia waziri kalemani kuwa atamaliza kazi kwa wakati kwani mpaka sasa amefikia aslimia 96 ya kazi yote iliyopo kwenye mkataba wake