Na Ahmed Mahmoud, Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk, Hamis Kingwangalla amesema kuwa hatuwezi kushuhudia sekta ya utalii ikipigwa na janga la Covid – 19 wakati kunamianya mbalimbali ya kuifungua sekta hiyo kwa kujadili mambo mbalimbali yanayopaswa kuchukuliwa ili watalii waje nchini.
Dk, Kingwangalla aliyasema hayo jana Jijini Arusha wakati alipokuwa akizungumza na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii nchini katika maandalizi ya mpango wa kupokea watalii baada ya janga la Covid – 19
Alisema sekta ya utalii itakuwa ni sekta ya kwanza kaamka hivyo kwa tafiti mbalimbali zinazoendelea na ikumbuke sekta hii ni sekta nyeti inayoingiza fedha nyingi za kigeni.
Alisema ni vyema sasa tujadiliane jinsi ya kuweka mambo mbalimbali ili kuifungua sekta ya utalii ingawa si jambo rahisi maana sekta hii imeathirika sana na ugonjwa huu hivyo lazima tujadili ili kuweka mikakati ya kuweka mbele yetu na baadaye tufungue milango ya kibiashara
“Tunakila sababu ya kujenga imani katika soko hili la utalii ikiwemo upimaji wa Corona kwa wageni wetu na jinsi ya kudhibiti sababu hatutaki tumwambukize virusi mtalii na sisi tusiambukizane”
Lazima tuangalie msingi ya afya iliyotolewa na inayotolewa na sekta za afya tuonaona nchi mbalimbali zimeanza kufungua mipaka yake na sisi lazima tuwe na viwango vibavyitakiwa ili kuwahudumia watalii wataokutwa na virusi tutawahudumiaje
Alisisitiza ugonjwa huu upo hivyo ni lazima sasa kutafuta mbinu zaukuhakikisha tahadhari mbalimbali za kudhibiti ugonjwa huu ikiwemo kuhakikisha tunajaribu kufanya utalii kwa tahadhari kubwa na kuzingatia maelekezo yote yanayotolewa na wizara husika.
“Haya tutakqyoyajadili lazima tuweke imani na kufuata muongozo itakayokubaliwa na serikali ikiwemo kuweka viwango vinavyotakiwa hivyo ni lazima tujadili jambo hili kwa kina na kisha kesho (jumanne) nitaongea kwa kina na vyombo vya habari ili kusema yale tuliyokubaliana “
Sekta hii imeathirika sana kwa familia zinazotegemea utalii sekta binafsi, mahoteli na sehemu nyingine hivyo lazima tujadiliane na kuyafikisha katika mamlaka zinazohusika
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Profesa Adolf Mkenda alisema kikao hicho ni muhimu na ni lazima watu wawe wazalendo katika kuhakikisha sekta ya utalii inanyanyuka tena
Kikao hicho kinashirikisha washiriki kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) , Mamlaka ya Hifadhi ya Njiro (NCAA) , Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (Tawa) Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Uhamiaji.