Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe ,akisisitiza jambo wakati akizungumza na viongozi kutoka mikoa inayolima zao la Kahawa hapa nchini kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe akieleza jambo wakati akizungumza na viongozi kutoka mikoa inayolima zao la Kahawa hapa nchini kikao hicho kimefanyika leo jijini Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti,akizungumza kwenye kikao cha viongozi kutoka mikoa inayolima zao la Kahawa hapa nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Kaim Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Prof. Jamal Adam,akifafanua jambo kwenye kikao cha viongozi kutoka mikoa inayolima zao la Kahawa hapa nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Wakulima wa Kahawa Kagera(KCU) Bw.Edson Rugaimukama,akizungumza kwenye kikao cha viongozi kutoka mikoa inayolima zao la Kahawa hapa nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa (KDCU Bw.Osca Domonick akizungumza kwenye kikao cha viongozi kutoka mikoa inayolima zao la Kahawa hapa nchini kilichofanyika leo jijini Dodoma.
…………………………………………………………………..
Na. Alex Sonna Dodoma
Serikali imemuagiza Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Nchini Dkt. Benson Ndienge kuwachukulia hatua za kisheria watu waliyoleta hasara katika vyama vya Ushirika vya Chama Kikuu cha Wakulima wa Kahawa Kagera(KCU) na Chama Kikuu cha Ushirika cha Wakulima wa Kahawa (KDCU) ili kufanyike uchunguzi wa upotevu wa bilioni saba.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe wakati akizungumza na viongozi kutoka mikoa inayolima zao la Kahawa hapa nchini.
Mhe. Bashe amesema kuwa kila aliyeshiriki katika kuleta hasara katika vyama hivyo wakamatwe na kupelekwa katika vyombo vya sharia ili hatua kali kuchukuliwa juu yao ili kupata kujua namna ya kurejesha deni la bilioni saba.
Aidha Mhe. Bashe amesema kuwa Benki ya Kilimo nchini inatakiwa kuhakikisha inashusha riba kutoka asilimia 11 hadi tisa kwa Mkulima wa Kahawa kupitia vyama vya KCU na KDCU ili kutoa nafasi kwa mkulima kuweza kunufaika na zao hilo.
Hata hivyo Bashe amesema lengo la kuitaka benki hiyo ishushe asilimia hizo ni kutaka wakulima waweze kupata mikopo katika Benki hiyo ambayo itawasaidia katika kuendesha Kilimo cha Kahawa.
“ serikali haizuii sekta binafsi kwenda kununua kahawa,isipokuwa imewakataza kwenda kununua kwa mkulima moja kwa moja” amesisitiza.Bashe
Mhe Bashe amesema kuwa vyama vya ushirika na uongozi wa benki wanatakiwa kuanndaa mfumo maalum wa mkulipa kulipwa ndani ya masaa 48.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti,ametoa wito kwa watendaji wa vyama vya ushirika kuaandaa mfumo mzuri wa wakulima kulipwa stahiki zao kwa usawa bila kucheleweshewa.
Kwa upande wake Kaim Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Prof. Jamal Adam,amesema kwa mnunuzi wa kahawa anuue kahawa kwa mkulima kwa bei iliyoelekezwa ili mkulima kupata haki stahiki zake.