WAZIRI wa Nishati Dkt Medard Kalemani katika akikata upete kuashiriki kuwasha umeme kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani Korogwe wakati wa ziara yake katika wilaya za Lushoto,Handeni na Korogwe mkoani Tanga iliyokuwa
inalenga kutembelea kwenye maeneo yanayofanyiwa kazi na wakandarasi
kupitia mradi wa Rea awamu ya tatu unaoendelea ambao unatarajiwa
kukamilika mwezi June mwaka huu kulia ni Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Mhandisi Peter Kanuti Magari
WAZIRI
wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto akizungumza na wananchi wa
Kijiji cha Kweisasu Kata ya Sindeni wilayani Handeni mara baada ya
kuwasha umeme katika eneo la Shule ya Msingi Kweisasu wakati wa ziara
yake kulia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe
WAZIRI
wa Nishati Dkt Medard Kalemani akiwasha umeme kwenye moja ya nyumba
zilizopo kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani Korogwe wakati wa ziara
yake kushoto anayeshuhudia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Korogwe Rahel
Mhando kulia ni mzee mwenye nyumba hiyo
WAZIRI
wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto akizungumza na mzee wa nyumba
aliyowasha umeme kwenye Kijiji cha Kwasunga wilayani Korogwe wakati wa
ziara yake
WAZIRI
wa Nishati Dkt Medard Kalemani akisisitiza jambo kwa Meneja wa Tanesco
wa Kanda ya Kaskazini Mhandisi Gaspar Msigwa kushoto na kulia
anayefuatilia kwa
umakini ni Meneja wa Tanesco Mkoa wa Tanga Mhandisi Julius Sabu wakati
alipowasilia eneo la Mkata wilayani Handeni kwa ajili ya kuanza ziara
yake mkoani hapa
wa Nishati Dkt Medard Kalemani katikati akipata maelezo kutoka kwa
Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Mhandisi Peter Kanuti Magari kuhusu
namna kituo cha Umeme Kilole kinavyofanya kazi wakati wa ziara yake ya
kushtukiza kwenye kituo hicho kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya
Korogwe Rahel Mhando
WAZIRI
wa Nishati Dkt Medard Kalemani kushoto akisisitiza jambo kwa
Meneja wa Tanesco wilaya ya Korogwe Mhandisi Peter Kanuti Magari wakati
alipotembelea kituo cha Umeme cha Kilole wilayani Korogwe wakati wa
ziara yake
………………………………………………………………………………
WAZIRI
wa Nishati Dkt Medard Kalemani ameagiza watu ambao watakaobainika
kuhujumu miundombinu ya umeme kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa kuiba
umeme au vifaa vyake wakamatwe na kuwekwa korokoroni ili waendelee na
utaratibu wa kisheria kusudi watu wengine wenye nia mbaya wajifunze na
kuachana na vitendo hivyo.
Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati wa
ziara yake katika wilaya za Lushoto,Handeni na Korogwe mkoani Tanga
iliyokuwa inalenga kutembelea kwenye maeneo yanayofanyiwa kazi na
wakandarasi kupitia mradi wa Rea awamu ya tatu unaoendelea ambao
unatarajiwa kukamilika mwezi June mwaka huu.
Kauli ya Waziri
huyo inatokana na Taarifa aliyopatiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya
Korogwe Rahel Mhando wakati alipofika kuwasha umeme kwenye Kijiji cha
Kwasunga wilayani humo ambapo alielezwa namna wizi wa umeme
ulivyokithiri kwenye wilaya hiyo.
Licha ya kuwasha umeme kwenye
baadhi ya vijiji kwenye wilaya ya Handeni,Korogwe na Lushoto pia alifanya
ufuatiliaji huo ili waweze kukamilisha kazi yao ndani ya muda huo na
amekwisha kutoa maelekezo kwa nchi nzima kwa wakandarasi wote
wanaoendelea kwa wale ambao watashindwa kumaliza kazi zao kwa mujibu wa
mkataba wake ambao unaishia mwezi June mwaka huu.
Maelekezo hayo
ni kwa wanaowasimamia wahandisi wote waanze kuwakata malipo yao ya
mishahara kwenye mikataba hiyo ambayo ni kwa mujibu wa mikataba ya malipo hayo
huku akiagiza ikikatwa wasikae nayo wairejeshwe kwa katibu mkuu hazina
ambaye ni mlipaji mkuu wa serikali ili fedha hizo zitumike kwa ajili ya
kuwaweka wakandarasi wengine ambao wataweza kumaliza kazi hizo.
“Ndugu
zangu ikibainika mtanzania amefanya hujuma ya kuiba umeme au vifaa
vyake mtu wa namna hiyo ni mhujumu achukuliwe hatua na viongozi wa
maeneo husika wala suala hilo sio la kumsubiri mweneja wa mkoa aje
ajiridhishe tunaomba ma DC msisite kutoa taarifa…
“Lakini kwa
wasiokuwa na nia njema ya miumbonu ya umeme wakamateni na wawekeni
Korokoroni na muendelee na utararibu wea kishereia kusudu watu wengine
wenye nia mbaya wajifunze kutoka kwenye tabia hizo ambazo sio nzuri kwa
ustawi wa shirika letu kwani wanakuwa wakirudisha nyuma juhudi kubwa
tunazozifanya “Alisema
Aidha Waziri Dkt Kalemani alisema wakati
mwengine kunapotokea wizi mameneja nao wanakuwa sehemu ya wizi huo kama
sio wao ni vibarua wao kwa sababu haiwezekani mtu ambaye haujui umeme
anafungua transfoma na kuiba umeme bila kujua taalumu ya umeme halafu
anaiba vifaa bila kuuungua lakini hatama kama sio mtaalamu wa tanesco ni
mtu aliyewahi kufanya kazi nanyi
“Nikisiria transfoma imeibiwa
mahali mtu wa kwanza kumchukulia hatua ni meneje wa eneo husika kwa
sababu yeye ndio mwenye jukumu la kusimamia wataalamu wake anaowapa kazi
lakini pia acheni kuwapa kazi vishoka kwani mnapowapa kazi matokeao
yake ndio hayo”Alisema Waziri Dkt Kalemani.
Akizungumzia suala
tatizo hilo mbele ya Waziri wa Nishati, Katibu Tawala wa wilaya hiyo
Rahel Mhando alimueleza kwamba kumekuwa na tatizo la wizi wa umeme hilo
tatizo bado lipo Korogwe ni kubwa huku akieleza kwamba wameweka mikakati
mbalimbali kama wilaya ya kuweza kukabiliana nalo
“Mh Waziri
amekwisha kutoa maelekezo na sisi kama wilaya tumepokea maelekezo hayo
na labda nisema kwamba kwa yoyote tutakayembaini anaiba umeme huo ni
hujumu uchumi atachukuliwa hatua kali na hatutawatamfumbia macho hilo
hazungumzia waziri tu bali hata Rais Dkt John Magufuli kila siku amekuwa
aksisitiza wizi wa miundombi ya umeme na kubuka umeme hilo wataendelea
kulifanyia kazi”Alisema
Hata hivyo Katibu Tawala huyo
alimshukuru Waziri kwa kufika kwenye kijiji cha Kwasunga kuwawashia
umeme ambacho kina kaya 204 ambazo zimekwisha kupata umeme lakini kwa
furaha wanamshukuru kwani mbali na vijiji vya awali zimeongezwa vijiji
tisa kwenye Jimbo la Korogwe Vijiji.
“Sisi kama wilaya
tunashukuru kwa sababu mmeendelea kutuongezea ukubwa upatikana umeme
Korogwe kwani tuna kituo cha kilole ambacho waziri ametembelea kuna
megawatts 5 zitaenda kuongezeka hivyo kitaongeza wigo mkubwa kwenye
matumizi ya umeme”Alisema Das Rahel.