Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo vifaa mbalimbali kwa ajili ya kupambana na Virusi vya Corona Wilayani humo jana. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindunzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Mika Likapakapa na Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Justice Kijazi.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, akimshukuru Kingu baada ya kupokea msaada huo. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindunzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Mika Likapakapa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga na Mkurugenzi wa wilaya hiyo, Justice Kijazi.
Mbunge Kingu (wa pili kushoto) akikabidhi risiti kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindunzi (CCM) wa Wilaya hiyo Mika Likapakapa aliyonunulia matairi ya gari linalotumika kwa kazi za chama. Kutoka kulia ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Noverty Kibaji, Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ikungi, Rehema Msumi, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapindunzi (UVCCM) wa Wilaya hiyo, Jafari Dude, Katibu wa UVCCM wa wilaya hiyo, Himidi Tweve na Mkuu wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo.
Msaada huo ukitolewa.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Justice Kijazi baada ya kupokea msaada huo.
Mbunge Kingu akikabidhi Sh.450,000 kati ya 900.000 alizotoa kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Ikungi eneo la Puma.
Viongozi mbalimbali wa Dini ya Kiislam wilayani Ikungi wakiwa kwenye hafla ya kupokea msaada huo.
Makamu Askofu Jimbo la Singida wa Kanisa la Tanzania Asemblies of God (T.A.G)-Puma, Caleb Maumbuka akimkaribisha Mbunge Kingu na msafara wake mara baada ya kuwasili katika kanisa hilo.
Waumini wa kanisa hilo wakiwa kanisani hapo.
Mkuu wa Kituo cha Watoto cha kanisa hilo cha Puma, Paul Mwini, akielezea mafanikio ya kituo hicho.
Mbunge Kingu akizungumza na waumini wa kanisa hilo.
Mbunge Kingu akimkabidhi Makamu Askofu Jimbo la Singida wa Kanisa la Tanzania Asemblies of God (T.A.G)-Puma, Caleb Maumbuka sh.400,000 kama mchango wake kwa kanisa hilo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindunzi (CCM) wa Wilaya hiyo Mika Likapakapa, akizungumza na waumini wa kanisa hilo.
Makamu Askofu Jimbo la Singida wa Kanisa la Tanzania Asemblies of God (T.A.G)-Puma, Caleb Maumbuka, akiwaombea viongozi wote waliofika kanisani hapo.
Msaada wa viti 20 ukitolewa Kanisa la FPCT la Kijiji cha Nkuninkana.
Na Dotto Mwaibale, Singida
MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo vifaa mbalimbali kwa ajili ya kupambana na Virusi vya Corona wilayani humo.
Vifaa vilivyotolewa na Mbunge huyo ni Ndoo pamoja na majaba ambayo yatasambazwa katika ofisi za serikali za vijiji, kata na magulio yote yaliomo Wilayani humo kama njia ya kuwakinga wananchi na Corona.
Katika hatua nyingine Kingu amemkabidhi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapindunzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Mika Likapakapa matairi ya gari yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki mbili na nusu kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2020.
Akikabidhi vifaa hivyo wilayani humo jana kwa ajili ya Corona Kingu alisema anaunga mkono jitihada za Serikali kwa ajili ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona
“Sisi kama wabunge niliona tunawajibu wa kuungana na Serikali dhidi ya gonjwa huu wa Corona,Mh.Mkuu wa Wilaya unaweza kuwa shahidi kwani Ugonjwa huu hata Sisi bungeni kuna baadhi ya wenzetu wameadhiriwa na Ugonjwa huu.”alisema Kingu.
Akikabidhi msaada wa matairi Kingu alisema baada ya kuona gari ya chama inachangamoto ya matairi aliamua kutoa kiasi hicho kidogo cha fedha kwa ajili ya kusaidia kununua tairi hizo ili gari hilo liweze kufanya kazi za chama hasa wakati wa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Mbali na msaada huo Kingu alitoa msaada wa sh.laki tisa kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (BAKWATA) Wilaya ya Ikungi, katika Kanisa la Tanzania Asemblies of God (T.A.G.) Puma alitoa Shilingi laki nne na Viti 20 katika Kanisa la FPCT la Kijiji cha Nkuninkana.
Akizungumza wakati akipokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo alimpongeza Mbunge huyo kwa msaada huo wa kuunga mkono jitihada za Serikali dhidi ya mapambano ya Corona na kuwa Rais John Pombe Magufuli amefanya jitihada nyingi ikiwa ni pamoja na kuzifunga shule na kuwa Serikali katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Corona imeweza kuwafikia viongozi wote kuanzia ngazi ya vijiji.
“Na Serikali imetoa vifaa tiba vyote na kwa Wilaya ya Ikungi Kituo cha Afya Kata ya Ihanja kimetengwa kwa ajili ya kupokea washukiwa wa Corona na Vituo vingine 46 vimetengwa kwa ajili hiyo.”alisema Mpogolo
Mpogolo ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kutoa taarifa kwa wafanyabiashara watakao kiuka kufuata bei elekezi ya sukari ya Sh.2,900 iliyopangwa na Serikali ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.