Naibu Waziri wa maji, Mhe.Juma Aweso wakati akizungumza leo jijini Dodoma na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji
Naibu Waziri wa maji, Mhe.Juma Aweso wakati akisisitiza jambo wakati akizungumza na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji
Kaimu Mkurugenzi Mkuu EWURA,akizungumza wakati Naibu Waziri wa maji, Mhe.Juma Aweso alipokutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji
Mkurugenzi wa Udhibiti Uchumi Bw.Nzinyangwa Mchany akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa maji, Mhe.Juma Aweso (hayupo pichani) alipokutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji
………………………………………………………………………….
Na.Alex Sonna, Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetakiwa kuhakikisha inadhibiti bei za Ankara maji nchini zinazopandishwa kiholela na kubambikiwa Ankara kwa wananchi zinazofanywa na mamlaka za maji nchini bila kupata kibali kutoka EWURA na kutoa elimu kwa wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa maji, Mhe.Juma Aweso wakati akizungumza na Menejimenti ya EWURA kuhusu malalamiko ya wateja wa maji nchini kuhusu Ankara za Maji.
Mhe.Aweso ameitaka EWURA kuwarejeshea huduma za maji wateja wote nchini waliokatiwa maji kwa makubaliano ili waweze kupata huduma hiyo katika kipindi hiki cha kupambana dhidi ya ugonjwa wa Homa ya mapafu inayosababishwa na Virusi vya Corona(COVID 19).
“Taifa liko katika mapambano na vita dhidi ya Corona, ugonjwa unaua kama yanavyouwa magonjwa mengine kikubwa ni kuchukua tahadhari na kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam, silaha pekee ya kukabiliana nayo ni maji tiririka na sabuni, sasa tunaagiza warejesheeni wananchi maji, mliowakatia kwa kuweka utaratibu mzuri wa kulipa madeni yao,”amesema Mhe.Aweso
Aidha Mhe.Aweso amesema licha ya Mambo mazuri na kazi kubwa inayofanywa na EWURA ila bado kuna matatizo na changamoto ambazo zinahitaji kupatiwa ufumbuzi wa kina ili kutoa huduma Bora kwa wananchi na hasa masikini.
“Mnafanya kazi nzuri lakini nataka nisiwapake mafuta maana haitawasaidia nawaeleza ukweli kuna malalamiko makubwa, Hali inayosababishwa ninyi muonekane kama taasisi ya kutoa tunzo na kushindwa kushughulikia na kero hizo,”amesema Mhe.Aweso
Aidha amebainisha kuwa, zipo mamlaka ambazo ni vinara kwa kuwabambikia na kuwapandishia wananchi bei za maji kiholela, akiwataka EWURA kuhakikisha wanafikisha ripoti ya mamlaka za aina hiyo wizarani ili ziweze kuchukuliwa hatua stahiki maana wizara ndio yenye kauli ya mwisho.
Pia Mhe. Aweso amesema kuwa changamoto kubwa ni elimu, EWURA hawajafanya kazi ya kutoa elimu kwa watumiaji wa maji, juu ya wajibu na haki yao pia kwa mtoa huduma Jambo ambalo litazaidia kuondoa malalamiko tofauti na hivi sasa ambapo wananchi wanapata haki ya kutumiwa Ankara kwa njia ya simu bila ushirikishwaji.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira, Titus Safari, amesema kuwa EWURA, imefanikiwa kutoa jumla ya leseni 119 katika kipindi cha Juni 2019.
Bw.Safari amesema kuwa EWURA imekuwa ikifanya ukaguzi kwa mamalaka za maji nchini zisizopungua 50, na kutoa maelekezo ya kuboresha na kuongeza ufanisi katika kutoa huduma Bora kwa wananchi.