………………………………………..
Na.Silvia Mchuruza,Bukoba
Mamlaka ya utabili wa hali ya hewa mkoa wa kagera TMA imewataka wananchi waliojenga kandokando na ziwa victoria kuchukua tahadhari kutokana mvua zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya mkoa huo.
Aidha ametoa agalizo kwa wilaza za Missenyi na Bukoba ambazo zimekubwa na adha ya mafuriko na kusababisha baadhi ya kaya kutafutiwa hifadhi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa TMA Mkoa wa Kagera Bw.Stephen Malunde wakati akizungumza na mwandishi wetu amesema kuwa kutokana na utabiri uliotolewa inatarajia kunyesha mvua katika ya wiki ya kwanza na ya pili mwezi huu huku wiki ya tatu na ya nne itapungua kidogo.
”Hivyo niwaombe wananchi kuendelea kuchukua tahadhari maana hata kama utabiri utaonyesha mvua kupungua inaweza kutokea siku moja mvua ikawa nyingi na kusababisha mafuriko”amesisitiza Bw.Malunde
“Kuhusu ziwa Victoria kujaa maji na kusababisha nyumba za wananchi zilizoko kandokando mwa ziwa hilo kujaa maji inawezekana suala hili limesababishwa na mvua za vuli zilizonyesha juu ya wastani kuanzia mwezi wa kumi hadi wa 12 mwaka jana, lakini inawezekana hiyo sio sababu pekee”amesema BW. Malunde.
Baadhi ya wananchi wamezitaka mamlaka zinazohusika kuchunguza sababu za ziwa hilo kujaa na kusababisha maji kuingia katika makazi ya watu, lakini pia wamewasihi wananchi wenzao kuacha kujenga karibu na vyanzo vya maji.