Home Mchanganyiko Wakala wa  huduma za misitu Tanzania (TFS) yakabithi miche 5,000  ya kivuli...

Wakala wa  huduma za misitu Tanzania (TFS) yakabithi miche 5,000  ya kivuli .

0

Mbunge wa Jimbo la Longido ,Dokta Steven Kiruswa akiotesha mti  mara baada ya kupokea msaada huo kutoka kwa Wakala wa huduma za misitu Tanzania ( TFS ).(Happy Lazaro)

Anayehifadhi miche ni Afisa mawasiliano na Mkuu wa safu ya Olmotonyi ,Lilian Mziray akipanga miti hiyo mara baada ya kuikabithi wilayani Longido.(Happy Lazaro)
Aliyeko kushoto ni Mhifadhi mkuu wa shamba la miti Meru/Usa ,Robert Faustine akimkabithi miche ya kivuli Mbunge wa jimbo la Longido ,Dokta Steven Kiruswa(Happy Lazaro)
****************************
Happy Lazaro,Arusha.

Arusha.Wakala  wa huduma za misitu Tanzania (TFS) imekabithi Miche 5,000  ya kivuli aina ya Acasia Mangifera kwa ajili ya utunzaji wa mazingira katika wilaya ya Longido na kuweza kukabaliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Akizungumza wakati wa kukabithi miche hiyo wilayani Longido,Mhifadhi Mkuu wa shamba la miti Meru/USA , Robert Faustine alisema kuwa,miti hiyo ya kivuli  itasaidia sana kutunza mazingira hasa katika ukanda huo  wa ukame  na kuweza kukabaliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Faustine alisema kuwa,zoezi la utoaji miche  hiyo ni zoezi endelevu ambapo mwaka Jana walitoa miche mingine Elfu tano kwa wilaya hiyo kwa ajili ya kukabiliana na ukame ambapo maendeleo yake ni mazuri sana kwani wananchi wameweza kuitunza .
“tumeona mahitaji ya wananchi wa Longido hivi Sasa ni kuhitaji miti ya matunda ili waweze kunufaika na matunda pia nje ya miti ya kivuli,tutalifanyi kazi hilo lengo letu likiwa ni kuhakikisha utunzaji wa mazingira unaendelezwa katika wilaya hii.”alisema Faustine.
Mbunge wa Jimbo la Longido ,Dokta Steven Kiruswa alishukuru kwa msaada huo kwani umekuja muda muafaka ambao wilaya hiyo ipo katika kampeni ya kuifanya Longido kuwa ya kijani .
Alisema kuwa,uwepo wa miche hiyo 5,000 zitagawiwa kwa Taasisi ,makampuni ,mashirika ,mashuleni na kwa wananchi ambapo wataweka mkakati wa kuandikisha majina kwa kila atakayechukua na mawasiliano yao ili waweze kufuatiliwa kwa karibu utunzaji wao na maendeleo ya Miche hiyo kwa ujumla.
Naye Afisa mawasiliano na Mkuu wa safu ya Olmotonyi ,Lilian Mziray aliwataka wananchi hao wa Longido kuitunza vyema miti hiyo ili iweze kubadilisha sura na taswira ya Longido kwa ujumla.
Mziray alisema kuwa,mtu akikupa miti na sawa na amekupa uhai kwani miti ni urithi mzuri sana unafaa kwa matumizi mbalimbali  hasa katika kukabiliana na ukame katika maeneo hayo.
Mwisho.