Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd, Ndugu Leonard Mahenda alikabidhi kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya corona Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium mbele ya mkurugenzi wa Mji wa Mafinga
Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd, Ndugu Leonard Mahenda alikabidhi kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya corona Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium
Baada ya kupokea mashuka 120 kutoka katika kampuni ya Qwihaya General Enterprises Ltd, Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Jamuhuri Willium ameishukuru kampuni hiyo na kuwaomba wadau wengine kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na ugonjwa wa Covid 19. Jana Mkurugenzi wa Qwihaya General Enterprises Ltd, Ndugu Leonard Mahenda alikabidhi kuunga mkono mapambano dhidi ya virusi vya corona. Mbali na msaada huyo, kampuni hiyo imefanikiwa kuikabidhi Serikali ya mkoa wa Iringa, vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh10 milioni yakiwemo mavazi 20 ya madaktari, matenki 60 ya kuhifadhia maji, barakoa na vitakasa mikono. “Kipekee nimshukuru ndugu yetu Qwihaya kwa msaada huu, mashuka haya yatatusaidia, wito wangu kwa wadau wengine tuungane mkono ili tuweze wote kwa pamoja kulikabili janga hili,” amesema DC wa Mufindi. Awali, Ndugu Mahenda alisema bado kuna vifaa vingine vimeandaliwa kwa ajili ya kuikabidhi wilaya hiyo katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo. “Bado tuna vifaa ambavyo tumeandaa kwa ajili ya halmashauri yetu ambavyo tutaleta kuendelea kukabiliana na ugonjwa huu, niwaombe wadau wengine waweze kujitokeza kukabiliana na ugonjwa huu,” amesema Mahenda.
|