…………………………………………………..
Na Magreth Mbinga,Dar es Salaam
Kuanzia kesho tunakamata wafanyabiashara wote wanaouza sukari kwa bei ya juu tofauti na iliyotolewa na Serikali.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda wakati akifanya ziara katika wilaya ya Kigamboni kukagua uboreshaji wa awamu ya pili ya daftari la kudumu la mpiga kura.
Makonda amesema hakuna sababu ya kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kupandisha bei ya sukari ambapo bei elekezi ya Serikali ni shilingi 2600 kwa kilo moja lakini watu wanauza hadi sh 3500 kwa kilo.
Aidha amewataka wananchi wasitumie hotuba ya Mh Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kusambaza taarifa mbaya na zakupotosha jamii ya Tanzania.
“Lengo la Mh Rais kupima sampuri za wanyama na matunda ni kukagua kipimo ambacho kinatumika kupima ugonjwa wa Corona na sio wanyama na mimea imeathirika na ugonjwa huo kuleni matunda kwani yanajenga afya ya mwili” amesema Makonda.
Hata hivyo Makonda amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwapatia heshima wananchi wa Dar es salaam kwa kuwapatia ruhusa waendelee kufanya kazi kwasababu wananchi wengi wanategemea watoke ili wapate pesa ya kula kwa siku.
“Tusimuangushe Rais Magufuli najua wapo baadhi ya watu waliotaka mji ufungwe ili tusimuangushe Rais watu tufate maelekezo ya wizara ya afya ili kulinda heshima ya kauli yake” amesema Makonda.