Afisa mwandikishaji ambaye ndio Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Bwana Aron Kagurumjuli akizungumza na watumishi hawapo pichani waliokuwa kwenye mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura katika shule ya msingo Osterbei.
Watumishi wa BVR Oparetas Kts na waandishi wa saidizi wakiwa kwenye mafunzo ya namna ya kutumia mashine hizo pindi watakapokuwa kwenye majukumu ya kuwahudumia wananchi watakaofika kuhakiki taarifa zao ili waweze kupata kitambulisho cha mpiga kura.
***************************
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeanza zoezi la uboreshaji awamu ya pili wa daftari la kudumu la mpiga kura ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye ndio Afisa mwandikishaji bwana Aron Kagurumjuli amesema wamejipanga vilivyo katika uboreshaji huo.
Kagurumjuli ametoa kauli hiyo wakati wamafunzo ya kuwajengea uwezo mbalimbali kuhusu namna kuwahudumiwa wananchi wanaokuja kuboresha taarifa zao sambamba na namna ya kutumia mashine wakati wa kuchukua picha kwa ajili ya kutoa vitambulisho.
Kagurumjuli amesema kuwa Halmashauri hiyo imejipanga vizuri katika mchakato huo na kwamba inategema matokeo mazuri ya mwitikio wa wananchi kama ilivyokuwa kwa awamu ya kwanza kutokana na kuwepo kwa ushikiano madhubuti baina ya AROKATA pamoja na watendaji wengine wa Hamashauri hiyo.
Ameongeza kuwa mchakato huo ni mahususi kwa ajili ya kuwapatia wananchi vitambulisho vyao