Mkurugenzi wa Airtel Money akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam baada ya Airtel Tanzania kuzindua huduma ya Timiza Akiba. Timiza Akiba imekua kwa asilimia 30 kwa miezi mitatu ya Disemba 2019 mpaka Machi 2020 na hivyo kutoa suluhisho ya kifedha kwa Watanzania kuwekeza fedha zao. Kulia ni Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando (Picha kutoka Maktaba)
……………………………………………………………………………………
Dar es Salaam
Ikiwa imekuwa kwa kiasi cha asilimia 30 kwa miezi mitatu pekee iliyopita, Timiza Akiba imeonyesha ni kwa kiasi ngani inaweza kuwa mkombozi kwa Watanzania kwa kujiwekea akiba ya fedha zao kwa njia rahisi, nafuu na salama kwa njia ya simu za mkononi.
Ikiwa imezindulia miaka miweili iliyopita kwa ushirikiano baina ya Airtel Tanzania kupitia huduma yake ya Airtel Money, Benki ya Letshego na watoa huduma ya teknolojia JUMO Tanzania, Timiza Akiba imekuwa ya kwanza Tanzania kwa kuwekeze fedha kwa njia ya kutumia simu za mkononi bure. Lengo ya Timiza Akiba ni kwa ajili ya Watanzania kujiwekea utamanduni wa kujiwekea akiba ili kufanikisha malengo yao.
Timiza Akiba inamfanya mteja wa Airtel kuweza kuwekeza fedha kidogo kwenye akaunti zao za Airtel kwa kuanzia kiasi kidogo cha Tzs100 mpaka Tzs5 milioni popote pale na muda wowote bila ya kwenda benki. Fedha hizo utunzwa kwenye akuanti maalum kwenye benki ya Letshego na kwa ambao Wateja watakaoamua kutenga na kuweka kiasi kidogo cha fedha zao kama akiba badala ya kutumia fedha zote watapata zawadi. Zawadi hii utengemea na akiba ya mteja iliyopo na vile vile Timiza Akiba inaunga mkono juhudi za serikali za kukuza utamanduni wa kujiwekea akiba.
Wakati mteja anapotaka kutoa fedha zake, hili ufanyika muda wowote bila kuwa na gharama zozote. Na hata hivyo, wakati wa dhararu, mteja anaweza kupata mkopo wa kupiga menu ya Airtel Money *150*60, changua 6, 1 na 3. Timiza Akiba inapatikana kwa wateja wote wa Airtel Tanzania kupitia simu zao za mkononi kwa simu ya aina yoyote ile bure kabisa. ‘Tuweke juhudi kubwa zenye ubunifu na teknolojia ya hali ya juu ili kutoa suluhisho la kifedha kwa Watanzania wote. Timiza Akiba inawafanya wateja wetu kuwekeza kwa kujiamini na kuepuka matumizi yasio ya lazima. Kuweka na kutoa fedha ni kwa njia ya simu za mkononi na hivyo kufanya miamala kufanya kwa njia salama na nafuu’, anasema mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda.
Mshirika Mkuu wa Timiza Akiba, benki ya Letshego Tanzania, ni moja kati ya benki ambazo ziko kwenye nchi 11 Barani Afrika na ambazo zimeorodhesha kwenye soko la hisa nchini Botswana na Namibia. Kaimu Mkurugenzi Letshego Bank Tanzania Andrew Tarimo anasema, ‘Letshego imejitolea kuwa suluhisho kwenye sekta ya kifedha nchini Tanzania na muhimu kuunga mkono wateja wetu wakati huu wa hali ngumu ya uchumi kwenye mapambano dhidi ya janga la COVID-19. Timiza Akiba ni njia ya mtandao kwa ajili ya kuweka fedha kwa wateja wetu na kuzitumia pale wanapoziitaji zaidi.
JUMO inajenga na kuendesha mifumo ya muda mfupi na mrefu ya bidhaa za kifedha kama vile Timiza Akiba. ‘Teknolojia yetu inapunguza matumizi ya utawala na sana sana mambo ya kiutawala na kupunguza gharama kwenye kuendesha masuala yanayohusu fedha na hivyo kufikia masoko mapya na wateja kupata huduma bora na za hali ya juu.’, anasema Mtendaji Mkuu JUMO Afrika Buhle Goslar. Ushirkiano wetu baina ya Letshego, na Airtel umepunguza vikwazo vya biashara na hivyo kuifanya Timiza Akiba kukua kwa haraka na zaidi kwa miezi mitatu iliyopita.
Mnamo Machi 2020, uwekezaji ndani ya Timiza Akiba ulifikiwa kiwango cha juu na kufikia rekodi ya asilimia 32 kwa miezi mitatu kuanzia Disemba 2019.. Ongezeko la ukuaji huu unatokana na kuongezeka kwa idadi ya wateja kwa mwezi wa Machi 2020 na namba ya wateja walio hai kwa asilimia 9 kwa mwezi huo ukilinganisha na miezi 6 ya awali. Vile vile, ongezeko hili inamaanisha kuwa idadi ya Watanzania wameamu kuwekeza, na zaidi kwa wafanya biashara ambao hali ya biashara inatengemea kupitia wakati mngumu.