*****************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wafanyakazi wa Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu yenye makao makuu yake jijini Arusha ,imejipanga kumuenzi aliyewahi kuwa rais na Jaji wa mahakama hiyo marehemu Augostino Ramadhani ,aliyefariki April 28 mwaka huu.
Jaji wa mahakama hiyo Blaiset Tchikaya ,amesema leo ofisini kwake kwamba marehemu Jaji Ramadhani alikuwa ni kiungo muhimu katika utendaji wa kazi wa mahakama hiyo kwa sababu alikua akijua mambo mengi hasa ya kijamii pamoja na sheria za kimataifa.
Amesema kuwa Jaji Ramadhani alikuwa rais wa mahakama hiyo kwanzia mwaka 2014 mpaka mwaka 2016 .
Amesema Mahakama hiyo katika kumuenzi Jaji Agustino Ramadhani juu ya utendaji wake imeteua kamati ya watu kumi na mmoja itakayojadili namna bora ya kutoa tuzo maalumu ya kumuenzi .
Kwa upande wake Faraji Mtolela, ambaye amewahi kufanya kazi pamoja Na marehemu Jaji Agustino Ramadhani ameseama jaji huyo alikuwa mkarimu, zaidi ya jaji ni sawa na baba kwao na pia alipenda watu wafuate maelekezo pamoja na taratibu zote za mahakama ya Afrika.
Naye mwandishi wa gazeti la the citizen Zephania Ubwani amesema kuwa Jaji Ramadhani ezi za uhai wake aliweza kutoa mchango mkubwa katika haki pamoja na utekelezaji wa sheria za haki za binadamu, pamoja na kutoa ushirikiano mkubwa kwa waandishi wa Habari.
Alisema kuwa Jaji Ramadhani wakati akiwa Rais wa Mahakama ya Afrika ya haki za binadamu na watu alikuwa mstari wa mbele kuona mahakama hiyo inakuwa na kujenga misingi ya kuheshimu utu na haki za binadamu.
ReplyReply allForward |