********************************
TAREHE 27.04.2020
TUKIO LA KWANZA: – MAUAJI.
TAREHE 26.04.2020 MAJIRA YA 22:00HRS, HUKO KATIKA
KIJIJI CHA IGENGE, KATA YA MBARIKA, WILAYA YA
MISUNGWI, MKOA WA MWANZA, ANASTAZIA ZAKARIA,
ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI YA 40
– 45, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA KITONGOJI CHA
BUHAJI, ALISHAMBULIWA NA MUME WAKE AITWAYE
LAURENTHERMAN, MIAKA KATI YA 50-55, MSUKUMA,
MKULIMA NA MKAZI WA KITONGOJI CHA BUHAJI, KWA
KUPIGWA NA KITU KIZITO KICHWANI NA KUPELEKEA
KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO. MARA BAADA YA KUFANYA
TUKIO HILO MWANAUME HUYO ALIAMUA KUNYWA SUMU
YA MADAWA YA KILIMO KWA LENGO LA KUJIUA, LAKINI
MAJIRANI WALISIKI KELELE NA KUFIKA NYUMBANI HAPO
NDIPO WALIMNYWESHA MAZIWA ILI KUNUSURU UHAI
WAKE NA BAADAE WALITOA TAARIFA POLISI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LILIFANYA
UFUATILIAJI WA HARAKA HADI ENEO LA TUKIO NA
KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KUMPELEKA MWANAUME
HUYO KITUO CHA AFYA CHA MBARIKA, LAKINI LEO TAREHE
27.04.2020 MAJIRA YA 07:15HRS ALIFARI DUNIA WAKATI
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.
CHANZO KINADAIWA KUWA MWANAUME HAKUWEPO
NYUMBANI KWAKE KWA KIPINDI KIREFU NA ALIPOREJEA
NYUMBANI HIVI JUZI ALIMWOMBA MKEWE TENDO LA
NDOA LAKINI MWANAMKE ALIKATAA AKIDAI MPAKA
WAKAPIME AFYA ZAO (UKIMWI), KWANI MWANAMKE
ALIKUA NA MASHAKA NA HALI YA KIAFYA YA MUME WAKE
NDIPO MWANAUME ALIKASIRIKA NA KUPELEKEA UGOMVI
ULIOPELEKEA VIFO VYAO.
MIILI YA MAREHEMU WOTE WAWILI IMEHIFADHIWA KITUO
CHA AFYA CHA MBARIKA KUSUBIRI UCHUNGUZI WA
DAKTARI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ITAKABIDHIWA
KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
TUKIO LA PILI: – KUTUPA WATOTO.
TAREHE 27.04.2020 MAJIRA YA 05:00HRS HUKO MTAA WA
MTAKUJA, KATA YA NYAMHONGOLO, WILAYA YA
ILEMELA, MKOA WA MWANZA, WATOTO WAWILI; WA
KWANZA JINSIA YA KIUME, ANAYEKADIRIWA KUWA NA
UMRI WA MWAKA MMOJA, AKIWA AMEVALISHWA FLANA
RANGI YA BLUE NA WAPILI JINSIA YA KIKE,
ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIEZI MITATU,
AKIWA AMEVALISHWA NGUO MOJA MWILI WOTE RANGI
NYEUPE, WAMEKUTWA WAKIWA WAMETUPWA KWENYE
SHAMBA LA MPUNGA/MAJARUBANI, WAKIWA KWENYE
MAZINGIRA MAGUMU LAKINI WAKIWA HAI, KITENDO CHA
KUWATUPA WATOTO HAO NI MIONGONI MWA MAKOSA
MAKUBWA YA KIKATILI DHIDI YA WATOTO NA
HAKIVUMILIKI.
WATU WOTE WALIOHUSIKA WATASAKWA POPOTE WALIPO
NA WATAKAMATWA NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.
WATOTO WAMEPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA YA
BUGANDO KWA MATIBABU NA HALI ZAO ZINAENDELEA
VIZURI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA WITO KWA
WANANCHI KUWA NA UVUMILIVU WANAPOKUMBWA NA
MIGOGORO YA KIFAMILIA NA WAPENDE KUHUSISHA
VYOMBO VYA KISHERIA KAMA MAHAKAMA NA TAASISI ZA
KIDINI KATIKA KUSAIDIA KUTATUA MIGOGORO HIYO.