Home Mchanganyiko THTU YATOA MAPENDEKEZO KADHAA YA KUKABILIANA NA ATHARI ZITOKANAZO NA JANGA LA...

THTU YATOA MAPENDEKEZO KADHAA YA KUKABILIANA NA ATHARI ZITOKANAZO NA JANGA LA CORONA KWENYE SEKTA YA ELIMU

0

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania(THTU) Dkt.Paul Loisulie (kushoto) akizungumza wakati akitoa taarifa yake kwa wanachama wake, wadau na umma wa watanzania wote nchini ikiwa ni sehemu ya kuungana na serikali katika kupigana vita dhidi ya Corona.

………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania(THTU) kimetoa wito kwa taasisi za elimu ya juu na vyuo vya kati kwa kuwataka kuonyesha umahiri wao wa kutumia TEHAMA ili vipindi viendelea kwa yale masomo yanayowezekana kwa njia ya mtandao.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa THTU Taifa Dkt.Paul Loisulie kupitia taarfa yake kwa wanachama wake, wadau na umma wa watanzaniawote nchini ikiwa ni sehemu ya kuungana na serikali katika kupigana vita dhidi ya Corona.

Dkt. Loisulie amesema kuwa waau husika kukaa na kusubiri tatizo liishe bila kuchukua hatu wenyewe ni kutojitendea haki wao kama wadau wa elimu nchini.

“Wito wetu kwa serikali ni kuwezesha taasisi hizi kuweza kufanikisha malengo hayo na kutoa msaada kwa taasisi za binafsi ambazo kwa wakati huu zinapitia wakati mgumu kutokana na janga hili la corona” amesema Dkt. Loisulie.

Dkt. Loisulie amesema kuwa Wizara zote zijielekeze katika kutengeneza taratibu na mazingira wezeshi yatakayoendelea kulinda mazingira ya kiuchumi na kijamii kwa mwananchi wa kawaida na pia kulinda shughuli za kiuchumi za biashara mbalimbali ili kulinda ajira za wafanyakazi wengi.

Aidha Dkt. Loisulie ameendelea kushauri kuwa mamlaka ya usimamizi wa usafiri wa nchikavu(LATRA) ikishirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha usalama barbarani iongeze usimamizi wa maelekezo ya watalamu wa afya katika usafiri wa umma kipindi hiki cha janga hili la corona.

“Pamoja na kazi nzuri ya Vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii vinatakiwa kuongeza ubunifu zaidi wa vipindi na Makala ya kusaidia mapambano dhidi ya janga hili” ameshauri Dkt. Loisulie.

Pia Dkt. Loisulie amesema kuwa mapambano dhidi ya corona si ya serikali , mtu mmoja au kundi moja tunahitaji kushirikiana kwa ukaribu zaidi ili ili kushinda vita dhidi ya corona ili watanzania na dunia kwa ujumla kuendelea na Maisha ya kila siku ya kutafuta kipato na kukuza uchumi wa Maisha yao na mataifa yao.