***********************************
Na Masanja Mabula ,PEMBA.
TIMU ya madaktari wa kichina walioko Hospitali ya Abdalla Mzee kisiwani Pemba , imetoa mafunzo kwa wauguzi na wafanyakazi wa hospitali hiyo lengo ni kuwawezesha kujikinga na virusi vya Corona wao na wagonjwa wanaokuja kupata huduma za matibabu katika hospitali hiyo.
Kiongozi wa timu ya madaktari hao Yuan Tongzhou alisema njia pekee ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona ni kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya.
Alisema iwapo kila mmoja atatimiza wjibu wake uwezekano wa kudhibiti kusambaa maambukiziya virusi vya Corona.
Yuan alifahamisha madaktari wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha wagonjwa wanaowapokea hosptalini hapo.
“Wauguzi kwanza mnajukumu la kujilina ninyi ili msipate maambukii ya virusi vya Corona nah ii elimu pia nawaomba sana ifikisheni kwa wananchi wanaokuja kupata huduma za matibabu hapa”alisema.
Katibu wa hospitali hiyo Ali Omar Mbarawa amesema kuwa elimu hiyo itawasaidia kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.
Alisema wafanyakazi wa hospitali wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwenye jamii inawazunguka ambapo wananchi wanatakiwa kuiga kutoka kwenu.
“Jamii ya vijijini tunafahamu kwamba inategemea kuona mifano kutoka kwa wauguzi na wafanya kazi wngine wa wizra ya afya , hivyo mafunzo yakawe dira na mwanga kwa jamii”alisisitiza.
Washiriki wa mafunzo hayo walisema elimu hiyo wataitumia na kuelemisha jamii kujua umuhimu wa kunawa na kuva barakoa ili kujikinga na ugonjwa wa COVID 19.
Timu ya madaktari wa kichina iliyoko katika hospitali ya Abdalla Mzee Mkoani Pemba imekuwa na kawida ya kutoa elimu kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo ni kuwaongezea uzoefu wa kazi.