Mkuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama ya Jiji la Arusha wakikagua madarasa kwenye Shule ya Sekondari Sombetini jijini Arusha Jana picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa kwenye Shule ya Sekondari Sombetini na kutoa siku Saba kwa mhandisi kuhakikisha wanaweka maji kwenye kituo Cha Afya huku akipongeza Ujenzi wa madarasa hayo na kutaka yakamilike kwa wakati picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Afisa elimu wa halmashauri ya Jiji la Arusha akitoa ufafanuzi mbele ya mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro wakati akipofanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na halmashauri ya Jiji hilo kwenye Shule ya Sekondari Sombetini picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
**************************
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa wilaya Arusha Gabriel Daqarro ametoa siku saba kwa kaimu mhandisi wa halmashauri ya jiji la Arusha Samwel mshuza kuweka maji katika jengo la upasuaji lililopo katika kituo cha afya Cha Muriet ili kuanza shughuli za upasuaji.
Akizungumza katika siku ya pili ya ziara yake alipotembelea kituo hicho katika kukagua ujenzi wa njia yakutembea kwa miguu inayounganisha majengo yote uliokamilika tarehe 4 March mwaka huu wenye ghara a ya shilingi milion 100 .
Mkuu huyo amesema kuwa anatoa siku saba kwa mhandisi huyo kwani maji ni sehemu kubwa ya kukwamisha wananchi kupata huduma ya upasuaji pamoja na shughuli nyingine ndani ya majengo hayo.
Akiwa katika shule ya sekondari Taret mkuu huyo amesema kuwa kabla ya mwaka wa fedha kuisha majengo hayo yawe tamekamilika ili kuanza mwaka mwingine wa fedha isiokuwa na Madeni ya nyuma.
” Haitaleta maana nzuri kuona tunaanza mwaka mwingine tukiwa na Madeni na kutokukamilisha baadhi ya majengo tunatakiwa kuanza mwaka na miradi mingine sio ya viporo”. Alisema daqqaro
Hatar hivyo mkurugenzi wa jiji Hilo Maulid Madeni amesema kuwa jiji limesimamisha shughuli zote za kawaida ili kuweza kukamilisha majengo yote .
” Mheshimiwa mkuu wa wilaya tunatambua wewe ni msaidizi wa Rais ndani ya eneo Hilo naomba nikuahidi jengo hili ndani yasiku 30 litakuwa limekamilika”.
Akizungumza mmoja wa wananchi wa eneo Hilo Abdala maguta amesema kuwa wanaishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha sekta ya elimu na kuwarahisishia wanafunzi wengi kutokwenda mashule ya mbali .