Moja ya bango lililochorwa na Vijana wa Kikundi cha ‘Visual Aided Stories, VAS’ likihamasisha jamii kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona-COVID-19. |
Moja ya bango lililochorwa na Vijana wa Kikundi cha ‘Visual Aided Stories, VAS’ likihamasisha jamii kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona-COVID-19. |
**************************
VIJANA wavumbuzi wa VAS (Visual Aided Stories), wamebuni njia ya kufikisha ujumbe kwa jamii kwa kutumia sanaa ya uchoraji. Hii ni katika kuunga mkono juhudi za Serikali kuhamasisha jamii kuhusu kujikinga na kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona-COVID-19.
Sanaa ya Umma kama wanavyoiita, ni uchoraji wa picha kubwa kwenye kuta zikiwa zimeambatanishwa na ujumbe kwa ajili ya jamii. Kikundi cha vijana VAS, kinachotumia vijana kipo Kata ya Kijitonyama Dar es Salaam.
Kikundi hicho kinajishughulisha na masuala mbalimbali ikiwemo uchoraji wa picha kubwa za rangi kwa lengo la kuhamasisha na kudumisha utamaduni, upendo, amani, na uzalendo wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.