LULU katika picha ya pamoja na msanii wa vichekesho Jaymond
Meneja uhusiano wa kampuni ya TECNO Bwana Eric Mkomoya
Elizabeth Michael akiwa na TECNO CAMON 15
**********************************
Kampuni kinara ya simu za mkononi ya TECNO, imezindua rasmi simu yake mpya CAMON 15 ambayo imesheheni sifa mbalimbali ikiwemo kamera ya nyuma yenye MP64 na mbele MP32 ambayo imewekewa teknolojia kubwa yenye uwezo wa kupiga picha mahali popote na wakati wowote.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo wiki hii jijini Dar es Salaam kupitia mitandao ya kijamii meneja uhusiano wa kampuni hiyo Bwana Eric Mkomoya, alisema simu hiyo itawasaidia sana watu wanaopenda kutumia kamera katika nyanja mbalimbali za maisha wakiwemo wafanyabiashara, wanamitindo, wanaopenda utalii wa kusafiri, wafanyabiashara za mitandaoni, waandishi wa habari pamoja na makundi mengine ya kijamii.
“Simu hii TECNO CAMON 15 ina sifa nyingi sana kubwa na zinazoweza kumridhisha mtumiaji, kamera yake ya nyuma ina MP64 na mbele ni MP32 lakini inatunza sana chaji. Kamera ya simu hii ina uwezo wa kupiga picha mahali popote na wakati wowote hata usiku” Alisema Mkomoya.
Aliongeza kuwa TECNO CAMON 15 ni tofauti na simu nyingine kwani hii inapiga picha kwa kuchukua eneo pana zaidi kutokana na kioo chake kikubwa hivyo hata kama mtu anapiga selfie ya zaidi ya mtu mmoja hahitaji kusogeleana kwa karibu hasa kipindi hiki cha janga la maambukizi ya virusi vya corona.
Wakati huohuo kampuni ya TECNO ilimtambulisha msanii wa Bongo muvi Bi. Elizabeth Michael maarufu LULU kuwa balozi wa CAMON 15. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Lulu alisema TECNO imefanya kazi nzuri na kwa wakati sahihi kuingiza CAMON 15 sokoni kwani simu hiyo ina uwezo mkubwa sana na anaamini itakata kiu ya watu wanaopenda kutumia kamera kama watu wa tasnia yake akiwemo yeye.
“Unajua maisha yetu kwa kiasi kikubwa yanategemea picha, wakati wowote na popote tunapokuwa tunafanya kazi zetu, tunategemea picha kupromoti kazi zetu , kwahiyo unakuta tunategemea kamera nzuri na yenye uwezo mkubwa, na kamera ya CAMON 15 binafsi nimeipenda sana” Alisema Lulu.
Pia Lulu alisema amevutiwa na muudo mzuri wa simu hiyo kutokana na umbo lake kuwa zuri na hivyo yuko tayari kujivunia popote atakapokuwa.
Wakati huohuo meneja mauzo wa TECNO Bi. Mariam Mohamed alizindua promosheni ya TECNO CAMON 15 nchi nzima ambapo kila mteja atakayenunua CAMON 15 atazawadiwa begi la TECNO au chombo cha kutunzia chakula maarufu ‘Lunch box’ ama kupewa vyote kwa pamoja.
“Ofa hii ipo mikoa yote kwenye maduka ya TECNO, kwahiyo tunawakaribisha sana wateja wote kwenye maduka yetu” Alisema Bi. Mariam.
TECNO imefanya uzinduzi wa simu yake kwa njia ya mtandao katikati ya juma ikiwa ni hatua muhimu ya kuepusha mikusanyiko katika kipindi hiki cha janga la Corona. Tayari TECNO CAMON 15 ipo kwenye maduka yote ya simu nchi nzima.