Mfanyakazi wa kituo Cha Mafuta Cha Puma kilichoko mtaa wa Jamhuri jijini Dar es salam akipulizia dawa baadhi ya magari yanayofika kituoni hapo kwa ajili ya kupambana na virusi vya Corona.(picha na Denis Mlowe).
******************************
NA DENIS MLOWE, IRINGA
KATIKA harakati za kupambana na virusi vya Corona nchini, Mkurugenzi wa kituo cha Mafuta cha Puma kilichoko mtaa wa Jamhuri
jijini Da es salaam, Muhammad Abri ameanzisha utaratibu wa kupuliza dawa za kuua vijidudu kwa wateja wote wanaokwenda kujaza Mafuta katika kituo hicho.
Akizungumza na mwanahabari hizi, Abri alisema kuwa utaratibu wa kupuliza dawa magari yanayofika katika kituo hicho cha Mafuta ni kila siku na kufanya hivyo kwenye kituo chote.
Alisema mlipuko wa virusi vya corona unaendelea kuathiri sekta zote duniani, mataifa mengi yameshindwa kupata jibu la kukabiliana na janga hivyo hakuna budi kuanza kupambana mapema visiendelee kuenea kwa kasi nchini kwani limekuwa janga kwa jamii.
Abri aliunga mkono kitendo cha serikali kutoa agizo la kufungwa kwa shule na vyuo vyote nchini kubaki vile vile hadi hapo Serikali itakapotoa tamko jingine.
Aidha alipongeza kitendo Cha serikali kuarisha maadhimisho ya Sherehe za Muungano, tarehe 26 Aprili 2020 pamoja na Sikukuu ya Wafanyakazi, Mei Mosi, 2020 ili kuepuka msongamano wa watu.
Abri alisema kuwa kitendo Cha Rais John Pombe Magufuli kusema watu wafunge na kusali ni jambo muhimu sana kwa sasa kwani kimbilio la kweli ni MUNGU hivyo wananchi watumie wakati huu kuweza kuomba na kufunga tuweze kuondokana na gonjwa hili.
Alitoa wito kwa wadau wengine wa vituo vya Mafuta kupuliza dawa ili kuwakinga wateja wao kuenea kwa virusi vya corona nchini.