Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Milos Lupa akitoa maelezo kuhusu utendaji wa NFRA wakati wa ziara ya kikazi ya katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akisisitiaz jambo wakati wa kikao kazi na Watendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA). Mwingine pichani ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Milos Lupa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya akisisitiaz jambo wakati wa kikao kazi na Watendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA). Mwingine pichani ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Milos Lupa.
Sehemu ya watendaji wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Ndg Gerald Kusaya wakati wa kikao kazi kilichofanyika NFRA Makao Makuu Jijini Dodoma.
Na Mathias Canal, NFRA-Dodoma
Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) imeanza kujipanga kuanza kununua mazao ya nafaka kwa wakulima ili punde tu mazao yatakapovunwa shambani yaweze kununuliwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya akiba ya chakula.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Milton Milos Lupa amemuhakikishia katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo ya Kilimo Ndg Jerald Kusaya wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja NFRA Makao makuu Jijini Dodoma kuwa tayari wataalamu wapo mikoani kwa ajili ya kazi hiyo.
Lupa amesema kuwa msimu wa kilimo wa mwaka 2019/2020 NFRA itanunua mazao makuu matatu ambayo ni zao kuu la chakula Mahindi, Mpunga na Mtama.
Amesema kuwa lengo la serikali kuamua kununua mazao hayo matatu ni kujiimarisha vyema katika uhifadhi wa chakula ili inapotokea dharula ya chakula nchini kuwe na hifadhi ya mazao tofauti tofauti.
Akizungumzia lengo la Wakala kuanza kujipanga ili kununua nafaka mapema, amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kupata mazao bora kwa ajili ya kuhifadhi kadhalika kupata mazao mengi.