Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akipokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Corona kutoka kwa Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma, Dk Dickson Chilongani leo.
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi akizungumza wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona vilivyotolewa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma
Baadhi ya vifaa ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona vilivyotolewa leo na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma leo.
Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma, Dk Dickson Chilongani akizungumza wakati wa hafla ya kugawa vifaa vya kupambana na ugonjwa wa Corona.
…………………………………………………………………………………
Na. Alex Sonna, Dodoma
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amepokea vifaa vya kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa Corona vyenye thamani ya Sh Milioni 16.5.
Vifaa hivyo vimetolewa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dodoma ambapo Askofu wake Dk Dickson Chilongani amekabidhi vifaa hivyo ikiwa ni jitihada za kuunga mkono serikali katika mapambano ya ugonjwa huo.
, Katambi ameshukur kanisa hilo kwa mchango wao huo wenye thamani kubwa kwa serikali na wananchi wote wa Dodoma.
” Tunawashukuru sana viongozi wetu wa Kanisa kwa namna ambavyo mmeungana na serikali katika mapambano ya ugonjwa huu, tunawaahidi kwamba vifaa hivi vitawafikia wananchi wote waliokusudiwa hasa kwenye maeneo yenye mikusanyiko.
Katambi ametoa wito kwa wananchi waendelee kufuata masharti yanayotolewa na wataalamu wetu wa afya na viongozi wakuu, tutumie vitakasa mikono lakini pia tuepuke mikusanyiko isiyo na ulazima.
” Hakika Rais Magufuli ni wa mfano amevunja mbio za Mwenge, amevunja sherehe za Muungano na Sikukuu ya Wafanyakazi lengo likiwa kuepusha mikusanyiko lakini pia fedha zilizokua zimetengwa kwenye shughuli hizo amezipeleka kwenye mapambano ya Corona”Amesema Katambi.
Kwa upande wake Askofu wa Dayosisi hiyo, Dk Chilongani amesema kitendo cha Rais Magufuli kuruhusu watu kuendelea kuabudu kwenye nyumba za ibada ni ishara kwamba yeye ni kiongozi hasa aliyeletwa na Mungu.
Amesema Dayosisi ya Dodoma imekua ikihudumia Wilaya tatu za Dodoma, Bahi na Chamwino na kwamba vifaa hivyo vitagaiwa sawasawa kwa kila Wilaya.