*********************************
NA MWAMVUA MWINYI,CHALINZE
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze ,Ridhiwani Kikwete amekabidhi mabati 1,000 kwa halmashauri ya Chalinze ,pamoja na tanki za maji na mabeseni Tisa vyote vikiwa na gharama ya milioni 13.9.
Kati ya mabati hayo 600 yataelekezwa katika miradi ya halmashauri ya sekta ya elimu na afya na 400 yatapangiwa kazi na matakwa ya mfuko wa jimbo.
Akizungumzia kuhusu msaada huo ,Ridhiwani alieleza kuwa , shule ya sekondari Changarikwa inapatiwa mabati 90,Msata 90,Chamakweza mabati 90,nyumba ya mwalimu sekondari ya Lugoba mabati 30 na shule ya msingi Magome mabati 60, Msolwa 60,Kidogozero mabati 90 na Ruvu Darajani.
Alisema,matanki ya maji yanakwenda katika vituo vya afya,zahanati ili kujikinga na janga la ugonjwa wa corona.
Ridhiwani alieleza ,kwasasa jamii inapaswa kujihadhali na ugonjwa huo hivyo akaona umuhimu wa kutafuta mdau Shubash Patel ambae alitoa matanki tisa aina ya Kiboko pamoja na mabati kwa ajili ya kuezeka miradi ya afya na elimu jimboni hapo .
“Kuna maeneo ya mkusanyiko mahitaji bado ni makubwa ya ndoo za maji kwaajili ya wananchi kunawa maji ,kama pale mnada wa Bwilingu ,nilitembelea wiki iliyopita mahitaji ni makubwa ” alisema Ridhiwani.
Kutokana na hilo pia amempata mdau mwingine ambae atamsaidia kuleta ndoo 30 kwa ajili ya kulinda na corona pamoja na makopo ya rangi na gymsum:;anasema Ridhiwani.
Nae mkurugenzi wa halmashauri ya Chalinze, Amina Kiwanuka alimshukuru mbunge wa Chalinze kwa ushirikiano anaouonyesha katika kutatua changamoto za kimaendeleo .
Kwa upande wake ,meneja uajiri wa Kampuni ya Sayona ,Godlove Mngwamba alisema mbunge Ridhiwani alipeleka maombi ofisini kwao na kutokana na utekelezaji na uwajibikaji wake katika kuwatumikia wananchi wamekubali kusaidiana nae kutatua changamoto mbalimbali kwa jamii.
Alisema ,hawatasita kuwa karibu na jamii kwakuwa ni muwekezaji mkubwa na anapaswa kushirikiana na jamii .
Godlove alifafanua ,ugonjwa wa corona ni janga la kupambana nalo hivyo wametoa matanki ya maji na mabeseni kwa ajili ya kutumika kwenye zahanati na vituo vya afya.
Alisema ,kuhusu mabati wametoa mabati 1,000 vitu vyote vikiwa na gharama ya milioni 13.9.