**************************************
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imeongeza vituo vya Afya (25) Kwa Mkoa mzima, ambavyo vitaanza kuhudumia wagonjwa kesho tarehe 15.04.2020 ili kuongeza nguvu katika kubaini wangonjwa wenye maambukizi ya virusi vya Corona.
Hii ni baada ya kuwepo kwa wananchi wanaokwenda vituo vya afya na zahanati mbalimbali au kulazimika kununua dawa baada ya kupata homa au kujisikia vibaya na badae kukutwa wameathirika na Corona.
Hali hii inaongeza idadi kubwa ya watu kuwekwa karantini huku tukipoteza nguvu kazi ya wataalamu wetu wa Afya wakiwa miongoni mwakundi la watu waliyoambukizwa.
Vituo hivyo vya afya, Zahanati, pamoja na hospitali zitampokea mgonjwa mwenye dalili zote za ugonjwa wa Corona, kama vile homa Kali, mafua makali, n.k na kumchukulia vipimo badae watakapobaini hana malaria au maradhi mengine, watafanya mawasiliano moja Kwa moja na mahabara kuu ya Taifa ili kuja kuchukua sampuli na baadae kupima virusi vya Corona.
Hatua hii ni kuhakikisha mtu yeyote atakayebainika na Corona kusahidiwa na kuzuia kuendelea kuambukiza watu wengine, ikiwemo pia na kulinda wataalamu wetu wanaotoa *huduma za Afya wasipate maambukizi
Sambamba na hilo mtu huyo atalazimika kukaa katika kitu hicho cha afya mpaka pale mahabara kuu ya Taifa itakapodhiirisha Hana Corona atachiwa kuendelea na shughuli zake, na akikutwa na corona utapelekwa sehemu usika zilizotegwa kuwahudumia watu wenye ugonjwa wa Corona.
Pamoja na kuwa na mgawanyo wa vituo vya afya * kila wilaya kama mkoa tumetengeneza *timu tano kila wilaya na kazi yake ni kuja kukuhudumia popote pale unapopiga simu, unaweza kushidwa kutoka nyumbani kuja hospitali hivyo watafika haraka sana.
Napenda kushukuru sana, serikali ya Mh. Rais Dr. John Pombe Magufuli, Kwa kutoa kipaumbele Kwa mkoa wa Dar es salaam, Kwa kutupatia magari ya kubeba wagonjwa mawili mawili (2) kila wilaya na magali mengine mawili mawili (2) ya wataalamu wetu wa Afya kila wilaya.
Pia tunaendelea kumshukuru Waziri wa afya Kwa kutoa vitendea kazi mbalimbali Kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mwisho, nawasihi wananchi wa Dar es salaam kuzingatia mambo makuu matatu moja nikujenga mahusiona makubwa na mungu wetu pasina mungu hatuwezi kushida hii vita, pili kuchukua taadhari zinazotolewa na wataalamu wetu wa Afya, tatu nikuendelea kuchapa kazi na kueneza habari njema zinazotoa hofu Kwa watu wetu.